Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

» » ZILE PICHA ZA UTATA ZA SHILOLE NA NUH MZIWANDA ZILIZOVUJA MTANDAONI HIZI HAPA



KABANG! Picha za staa wa sinema na Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole Kiuno’ zinazomuonesha live akiwa chumbani tena kitandani kimahaba na mwandani wake, Nuh Mziwanda zimevuja, Risasi Jumammosi linazo kwenye makabrasha yake.
Staa wa sinema na Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole Kiuno’.
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Shilole, picha hizo walijipiga wenyewe wakiwa kitandani nyumbani kwa mwanadada huyo, Kinondoni jijini Dar.
Chanzo hicho kilidai kwamba picha hizo walijipiga baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwani kabla ya hapo wasingefanya hivyo.
Katika picha hizo zinazowaonesha wawili hao wakiwa katika mahaba niue, Shilole anaonekana akiwa amemlalia Mziwanda ambaye naye amejiachia vya kutosha.
‘Shilole’ akipozi kimahaba na mwandani wake, Nuh Mziwanda.
Habari za ndani zinadai kwamba mmoja wa watu wa karibu alishika simu ya Shilole kisha akajifowadia picha hizo ndiyo chanzo cha kumfikia sosi wetu huyo.
Baada ya kuzidaka picha hizo, gazeti hili lilimtafuta Shilole ambaye kwa sasa anakimbiza na ngoma yake mpya ya Namchukua ambapo alipopatikana kwa njia ya simu alisomewa mashitaka yake ndipo akafunguka namna alivyochezewa na mtu wa karibu yake.
‘Shilole’akiendelea kula ujana na mpenzi wake.
kimahaba na mwandani wake, Nuh Mziwanda“Kweli hizo picha ni zangu na Nuh (Mziwanda), tulijipiga kwa ajili ya kumbukumbu na tulikuwa na muda mrefu hatujiachia si unajua tena Mwezi Mtukufu?
“Unajua simu yangu haina password na nina watu wengi wa karibu so nahisi ndiyo wamezivujisha na nikimjua namtoa kabisa kwenye network yangu maana siku nyingine anaweza kunifanyia jambo kubwa baya.”
Mbali na hilo, Shilole amesema yupo kwenye mazoezi ya kufa mtu akitamba kwamba atamkimbiza vilivyo staa wa Nigeria, Yemi Alade watakapokutana jukwaa moja kwa ajili ya shoo kubwa kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini, Agosti 8, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Unakaribishwa Kusoma habari za udaku na za siasa kila siku, usikubali kupitwa, like page yetu ya swahilitz katika facebook na pia usisahau kutufollow katika instagra @swahilitz vile vile katika twitter @swahilitz1. unakaribishwa kutoa maoni yako hapo chini.PI

About Unknown

Habari karibu katika Blog hii, Tafadhali Like Page Yetu na Toa Maoni yako kuhusiana na kile unachokiona humu.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga