Siku chache baada ya wimbo wake wa Thats The Way uliojaa matusi yasiyoweza kuandikika gazetini kuanza kusambaa kwa kasi kwenye mitandao , msanii wa kitambo wa muziki wa kizazi kipya, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’ amefunguka kuwa halikuwa kusudio lake kuachia wimbo huo bali ulivuja kwa bahati mbaya mitandaoni.
Akipiga stori na Showbiz juzikati, Dully alisema kuwa wimbo huo aliomshirikisha mwanadada Maunda Zorro, aliurekodi miaka nane iliyopita kwenye studio yake ya Dhahabu Records na hakupanga kuutoa lakini kwa bahati mbaya ukavuja na kuingia mitandaoni.
“Siyo mpya, ni wa kitambo sana, nilirekodi miaka nane iliyopita nashangaa kwa nini watu wanafikiri ni mpya,” alisema Dully lakini alipoulizwa hata kama ni wa zamani kwa nini alirekodi wimbo wenye maneno ya kuhamasisha ngono, hakuwa na majibu.
Licha ya utetezi wake huo, wimbo huo unaonekana kuwa mpya kwani sauti ya Dully inafanana na ya kwenye nyimbo zake mpya za hivi karibun