Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

» » » » » LADY JAY DEE "SASA NI WAKATI WANGU"


Baada ya tetesi kuwa ameachana na mumewe, mwanamuziki Judith Wambura maarufu Lady Jaydee amesema leo anajitokeza kwa mara ya kwanza mbele ya mashabiki wake kwani wakati wa kufanya hivyo umewadia.
Mwimbaji huyo wa wimbo “Yahaya” anayemiliki tuzo 30 za muziki, amejigamba kuwa hivi sasa yupo bize na kazi, kwani anatarajia kuachia wimbo matata alioupa jina la “Forever” ambao utaambatana na uzinduzi wa video yake Novemba 28.
“Sina habari na mtu na nitaendelea kuwa komando, kilichopo watu wasubiri kuona nitawapa nini maana leo ndiyo naachia wimbo huu, nina mengi ya kuzungumza nao pale nitakapotambulisha kibao hicho, watege tu masikio yao,” alisema Lady Jaydee.
Alisema anataraji kwamba wimbo huo mpya utapendwa na mashabiki wake ikiwa ni moja ya mikakati yake kabambe ya kuwafikia washabiki kwa ukaribu zaidi.
“Watarajie burudani waliyoizoea, nitaachia wimbo wangu leo Jumatatu na video yake nitaizindua Ijumaa na mashabiki watakaohudhuria utambulisho huu watapata bahati ya kuiona video ya “Forever” kwa mara ya kwanza,” alisema Jaydee.
Jaydee aliyepata kutamba na vibao kadhaa kwa kipindi cha takriban miaka 14, amesema wimbo huo amemshirikisha mwanamuziki wa regge, Dabo ambaye pia ni mdogo wake.
“Ni wimbo wa mapenz ambao utabamba, kazi hii imetengenezwa na prodyuza yuleyule Man Water wa Combination Sounds,” alisema.
Alisema pamoja na muziki, ataendelea kuisadia jamii kama ambavyo amekuwa akifanya kila siku na mazingira yakiendelea kuruhusu. “Mahitaji ya jamii ni mengi ila kila kinachowezekana basi Lady Jaydee atafanya kama msaada wa madawati nilioutoa Shinyanga.”
Hata hivyo, nyota huyo hakutaka kuzizungumzia tetesi zilizoenea kuwa ameachana na mumewe.
Lady Jaydee amewahi kutamba na vibao kadhaa huku akiwa na albamu tano ikiwamo, Machozi (2000), Binti (2003), Moto (2005), Shukrani (2007) na The Best of Lady Jaydee (2012).

About Unknown

Habari karibu katika Blog hii, Tafadhali Like Page Yetu na Toa Maoni yako kuhusiana na kile unachokiona humu.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga