Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

» » » » MENINAH BADO ANAMTAKA DIAMOND PLATINUMZ


Mganga aliyejita-mbulisha kwa jina moja la Kimweri ameibuka na madai mazito kuwa ndiye aliyemng’arisha staa wa kike wa Bongo Fleva, Meninah Abdukareem ‘Meninah La diva’ hivyo kutoa siri nzito ambayo wengi hawakuijua.
Staa wa kike wa Bongo Fleva, Meninah Abdukareem ‘Meninah La diva’.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mganga huyo amekuwa akimfanyia ndumba msanii huyo ili arudiane na aliyekuwa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinum’.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, mganga huyo amekuwa akidai kwamba, huwa msanii huyo anatinga nyumbani kwake maeneo ya Mwananyamala-Komakoma jijini Dar kisha kumlilia shida yake akimtaka afanye juu chini kuhakikisha anamrudisha Diamond mikononi mwake.
 Meninah Abdukareem ‘Meninah La diva’ akipozi.
Baada ya kukisikia chanzo hicho, waandishi wetu walikwenda nyumbani kwa mganga huyo na walipomuuliza ishu hiyo alikiri Meninah kufika kwake ili kufanyiwa ndumba arudiane na Diamond.
“Yule msanii anayeitwa Meninah ambaye habari zilivuma kuwa anatoka na Diamond na kukanusha, huwa anakuja hapa kufuata tiba na kikubwa anachokitaka anataka nimvute Diamond ili warudiane,” alisema.
Meninah alipoulizwa kuhusu madai hayo aliruka kimanga na kudai hakuwahi kuwa na uhusiano na Diamond na wala hamjui mganga huyo.

About Unknown

Habari karibu katika Blog hii, Tafadhali Like Page Yetu na Toa Maoni yako kuhusiana na kile unachokiona humu.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga