Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

» » » NAFASI YA HIGH HEELS KWA MVUTO WAKO MWANAMKE



Kinadada wengi wanavaa viatu virefu kwa mazoea au wakati mwingine kwa kuona mwenzake amevaa na amependeza.
Kupendeza kwa mmoja kunaweza kuwashawishi wengi kujaribu kuvaa viatu hivi bila kujua kuwa vinaweza kubadilisha mwonekano wake kulingana na namna unavyoweza kuvimudu.
Kiatu hiki kinaweza kuongeza mvuto wako endapo utaweza kukimudu na kutembea nacho kwa uhuru bila kuwa na wasiwasi wowote.
Kuweza kuhimili viatu virefu kunamfanya mvaaji kuonekana mrembo na mwenye kujiamini. Ni viatu ambavyo vinaweza kuonekana kwenye mazingira yoyote isipokuwa kwenye michezo.
Tofauti na aina nyingine za viatu hivi inaweza kuvaliwa na nguo yoyote iwe sketi ndefu au fupi, gauni refu na fupi, suruali za kitambaa na jeans.
Kama unajiona huwezi basi usivae kabisa kwani vinaweza kukupotezea mvuto wako na kuwa kichekesho mbele za watu kutokana na namna utakavyoonekana ukihangaika nacho
Imeandaliwa na Elizabeth Edward

About Unknown

Habari karibu katika Blog hii, Tafadhali Like Page Yetu na Toa Maoni yako kuhusiana na kile unachokiona humu.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga