ALIYEKUWA mchumba wa msanii wa filamu Bongo, marehemu Sheila Haule ‘Recho’, George Saguda amefunguka kuwa picha za mwanadada huyo zimekuwa zikimfanya asiwe na hisia za kuwa na mwanamke mwingine.
“Tangu alipofariki Recho niko peke yangu na sina mpango wa kuwa na mwanamke mwingine, kwani kila ninapozitazama picha zake naumia sana,” alisema Saguda.
Saguda aliongeza kuwa, licha ya kwamba yeye ni mwanaume aliyekamilika lakini tangu mchumba wake alipofariki dunia hana hisia za kimapenz kwa mwanamke mwingine na akipata hali hiyo huzitazama picha zake hisia hizo hutoweka.