Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

» » » » PENNY APIGA KELELE ZA UCHUNGU BARABARANI



Prizenta wa Kituo cha Radio E-FM cha jijini Dar, Penniel Mungilwa ‘VJ Penny’ anadaiwa kukumbwa na mauzauza yaliyodaiwa ni mapepo na kujikuta akipiga makelele barabarani.


Habari kutoka kwa shuhuda wetu zilidai kwamba, ishu hiyo ilijiri maeneo ya Makongo jijini Dar es Salaam, juzikati wakati staa huyo akielekea msibani ambapo rafiki yake kipenz aitwaye Skitter alifariki dunia.

Chanzo hicho kilidai kwamba Penny alikuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kawaida, alipofika maeneo hayo aliegesha gari pembeni na kuanza kupiga kelele akilia kwa uchungu hivyo kuwaacha watu waliomshuhudia wakiwa midomo wazi wakitaka kujua kilichompata mtangazaji huyo. Mpashaji wetu huyo alizidi kueleza kwamba baada ya kama  dakika kumi, Penny aliondoa gari na kuendelea na safari.

Paparazi wetu aliponyetishiwa ishu hiyo alimtafuta Penny na kumuuliza kuhusu tukio hilo ambapo alisema alikuwa akienda kwenye msiba wa rafiki yake, alipokaribia kufika alipata uchungu ndiyo akatokewa na hali hiyo

About Unknown

Habari karibu katika Blog hii, Tafadhali Like Page Yetu na Toa Maoni yako kuhusiana na kile unachokiona humu.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga