Mchapaji wa India Vijay Singh anaweza
kuchapa zaidi ya maneno 100 kwa dakika
kwa kutumia vidole vyake 12.
Lakini Vijay, ambaye pia ana vidole 12 vya
miguuni kutokana na dosari yake hiyo ya
kimaumbile, anasema hawezi kupata kazi
katika nchi yake aliyozaliwa sababu waajiri
wanataka tu wanawake wenye mvuto.
Sasa anapanga kuhamia Uingereza kwa lengo
la kutafuta ajira baada ya kuwa amekataliwa
maombi yake ya kazi zaidi ya 50.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 48,
anayetokea Agra kaskazini mwa India,
alisema: "Wanataka wanawake wenye
mvuto, si wanaume wenye vidole 12."
Watu wenye dosari za kimaumbile
wanaonekana wenye bahati nchini India na
Vijay yuko kwenye hali nadra kutokana na
vidole vyake vya ziada kufanya kazi kama
kawaida.
Watu wengi wenye hali hiyo wana vipande
vichache vya tishu laini ambazo zinaweza
kuondolewa na mara chache huwa na
mfupa, lakini bila viungio.
Lakini licha ya kuwa na uwezo binafsi
'kwenye kompyuta' kutokana na zawadi
yake, hajaweza bado kupata kazi na sasa
anataka kusafiri kwenda Uingereza kwa
matumaini kutakuwa na kitu fulanu cha
kufanya, imeripotiwa.
Mchapaji mwenye kasi zaidi duniani ni
Michel Shestov. Anaweza kuchapa katika
lugha 27, na kuweza kufikia kasi ya herufi 17
kwa sekunde!
Shestov alisomea kuchapa katika jeshi la
Urusi, ambako alikuwa akichapa kwa hadi
saa nane kwa siku