Watu wanawapenda mastaa, wapo  wanaowapenda mpaka wanatamani wafanane nao, mara nyingi tumekutana na  hizi story za watu ambao wamekuwa wakifanya majaribio ya kujibadilisha  muonekano, maumbile yani ili tu afanane na staa wake anayempenda.
Jordan  James alitumia dola 150,000 (zaidi ya mil 270/-)  ili kujibadilisha  afanane na Kim Kardashian, safari hii ni Adam Guerra ambaye yeye  jitihada zake alikuwa akizifanya ili afanane na Madonna.
Pesa aliyotumia ni paundi 75,000/- (sawa  na mil. 210/-) na kutokana na ‘ukarabati’ ambao anataka kuendelea  kuufanya kwenye mwili wake mpaka zoezi likamilike kiasi cha pesa  kitakuwa kimefikia paundi 100,000/-
Adam anasema anavutiwa sana na Madonna ndiyo maana anafanya kila kitu ili afanane naye.
Madonna
“Nimewahi  kupanda jukwaani nikamuiga Madonna.. nilipata mashabiki wengi, nimekuwa  nikivutiwa naye kwa kila kitu, nimefanya maamuzi yangu binafsi kwa  kutumia hela zangu ili nifanane naye kutokana na map3nzi yangu kwake,  pia nimepanga kufanya ziara za kimataifa ili kuwadhihirishia watu jinsi  gani navutiwa naye“-Guerra
