Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

» » » SAKATA LA KUUMIA KWA MTOTO WA WHITNEY NA BOB BROWN, MCHUMBA WAKE MATATANI



Habari ambazo Vijimambo imezipata, Bobbi
Kristina alikutwa na michubuko ambayo
bado haijajulikana imetokana na nini japo
bado Polisi wanaendelea na uchunguzi ikiwa
Nick Gordon na rafiki yake waliokuwepo
kwenye tukio wakiwa wamehojiwa na polisi
wa jimbo la Georgia.
Polisi inajaribu kutafuta saa moja kabla ya
Bobbi Kristina kukutwa bafuni ni nini
kilichokua kikiendelea kati ya hao wapenzi
wawili. Vijimambo imepata taarifa Max
Lomas rafiki ya wawili hao aliyemgundua
Bobbi Kristina akiwa ameanguka bafuni,
alifika nyumbani kwao majira ya saa 3
asubuhi na kuwa na Nick Gordon kwa muda
huo bila ya kumwona Bobbi Kristina huku
akiambiwa alikuwa chumbani.
Mida ya saa 4 asubuhi alifika fundi wa
kutengeneza waya za TV na alikuwa akihitaji
kuingia chumbani kurekebisha tatizo hilo
wakati huo Nick Gorgon alikua hajulikani
alipo ndipo Max Lomas alipochukua jukumu
la kumwingiza fundi huyo chumbani
kufanya marekebisho hayo na Max kumkuta
Bobbi Kristina akiwa bafuni ameanguka
huku kichwa chake kikiwa kimeinamia chini
na Max kupiga ukelele wa kuomba msaada
ndipo Nick Gordon alipotokea na kujaribu
kutoa huduma ya kwanza kwa Bobbi
Kristina.
Max Lomas alisema nyumba ya wawili hao
ilionekana kama imepigwa deki na kujaribu
kusafisha alama za damu iliyokuwepo
kwenye sakafu. Habari zingine zinasema
Polisi wanataka kumhoji tena Max Lomas
kwa mara ya pili ili kuendelea kupata
ushahidi wa kutosha kama wawili hao
walikwaruzana na kupigana kulikopelekea
Bobbi Kristina kuishia kuanguka bafuni na
kuzimia.
Nick Gordon na Bobbi Kristina
wameishakuwa na ugomvi wa mara kwa mara.

source. Vijimambo.
mara huko nyuma.

About Unknown

Habari karibu katika Blog hii, Tafadhali Like Page Yetu na Toa Maoni yako kuhusiana na kile unachokiona humu.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga