Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

Majanga ONA Majanga!!!! Mpaka Kieleweke Leo!!


Kama kawaida, Cheka Upate Afya, leo nakuletea Picha niliyoipata katika mtandao wa kijamii huku ikiwa Commented ya Kwamba Mpare Utamjua Tu!!!! Walionaje hili?

Cheka Upate Afya, Waionaje Tathmini hii ya Elimu ya Bongo?!!!

-->

Hapo Vipi Mjomba? Kwa Hali hii Tutafika Kweli?!!!!!!!!!!

Angalia jinsi wanadamu wanavyokumbatiana kuepuka vishawishi "Holy Hug"




Kama picha inavyoonekana waionaje hii? Hapa cahji za vishawishi zitapita kweli? Definitely No!!!!

Angalia Jude Okoye alivyotandaza Dola akijiandaa kununua gari online

Kama anavyoonekana pichani, kaka mkubwa wa kundi la P squire akizimwaga zaidi ya dola za kimarekani 10,000 huku akiperuzi katika laptop gari gani jipya anunue. Mambo ya fedha hayo.

Bibi harusi afariki dunia saa moja kabla ya kufunga ndoa kanisani Tanga

-

->


Handeni. Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Bibi Harusi ambaye ni mkazi wa Chanika mjini Handeni, Levina Mmasi (23) amefariki dunia saa moja kabla ya ndoa yake kufungwa katika Kanisa la Katoliki la Roma Wilaya Handeni Jumamosi na hivyo kuilazimu kamati ya maandalizi ya harusi kujigeuza na kuwa ya msiba.
Kifo hicho kilichotokea Jumamosi mwishoni mwa wiki iliyopita, kimekuwa gumzo mjini Handeni huku wananchi wakisema kuwa ni tukio ambalo halijawahi kutokea katika wilaya hiyo.
Msemaji wa familia ya marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Firmin Mrimasha, alisema kuwa chanzo cha kifo cha Levina ambaye alijifungua mwanzoni mwa wiki iliyopita,ilikuwa ni homa aliyoipata ghafla siku ya Alhamisi na kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni na kukutwa na malaria na kisha kulazwa kwa matibu.
 “
Huyu bibi harusi alikuwa ametoka kujifungua, alikuwa na mtoto wa kiume kutokana na ujauzito wa miezi saba, ndipo ghafla Alhamisi akapata homa tukampeleka hospitali alikolazwa na baada ya kupata nafuu, aliruhusiwa Ijumaa.



“Baada ya kuruhusiwa akaanza maandalizi ya harusi na Jumamosi ambayo ndiyo siku ya ndoa yake, alijiandaa lakini ilipofika saa 8.05 akafariki dunia akiwa nyumbani akisubiriwa kwenda kanisani kufunga ndoa ambayo ilikuwa ifungwe saa 9.00,” alisema Mrimasha.
Alisema, “Inasikitisha sana ila imeshatokea yaani marehemu amefariki saa moja kabla ya ndoa yake na baada ya kifo hicho, mtoto wake naye alifariki muda mfupi baada ya mama yake kufariki dunia,” alisema Mrimasha.
Akizungumzia mkasa huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Harusi hiyo iliyogharimu Sh7.7 milioni, Abdi Kipacha alisema kuwa kwake ni tukio la kwanza kutokea tangu kuzaliwa kwake na kamwe hawezi kulisahau.
“Nilishazipangia kazi kamati za maandalizi, lakini ghafla tukapewa taarifa kuwa bibi harusi amefariki...Hatukuamini, ikabidi niwatangazie wanakamati wenzangu kuwa hakuna tena shughuli, bibi harusi amefariki,” alisema mwenyekiti huyo wa kamati na kuongeza:
“Kitu tulichokuwa tukisubiri ni kuambiwa bibi harusi angefika saa ngapi, lakini ghafla tukapewa taarifa za kifo, ilikuwa ni vigumu kuamini lakini ni kweli imetokea na inasikitisha kwani si jambo la kawaida,” alisema Kipacha.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na wanandugu ni kuwa marehemu alikuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi Nndawa mkoani Lindi na kwamba alikuwa katika kundi la walimu wa ajira mpya ambayo hadi mauti yanamkuta alikuwa hajapokea hata mshahara wake wa awali.
Akizungumzia hali hiyo, Padri aliyekuwa afungishe ndoa hiyo, Max Sabuni wa kanisa hilo Katoliki Handeni alisema:       “Nimesikitishwa na tukio hili kwa kuwa halikuwahi kunitokea...Kilichobaki ni wanandugu kuwa watulivu kwa kuwa Mungu amechukua kiumbe wake kwa muda alioupanga.”
Aliwataka ndugu, jamaa na marafiki kuwa na subira katika kipindi hiki cha majonzi.
Source: Mwananchi

Mcheki alivyokuwa Kipindi hicho, unamwonaje na sasa?



Hivi ndivyo Beyonce alivyompongeza jay z, kwa kuiweka picha hii Istagram.

Angalia Mh. Sumaye Akiselebuka Katika Send Off ya Natasha


Wiki iliyopita, kulikuwa na Send off party ya Suzan Lewis, Maarufu kama Natasha, Muigizaji mkongwe wa filamu za Tanzania na Mama Mzazi wa Muigizaji Yvone Sherry maarufu kama Monalisa. Sherehe hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa wazi, miongoni mwa watu waliojitokeza kuinogesha ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Mh. Fedrick Sumaye, kama anavyoonekana akiselebuka hapo pichani.

Angalia Picha za Sherehe za Siku ya Jeshi la Nigeria

--> Angalia jinsi tarehe 6 July mambo yanavyokuwa huko Nigeria. Safari hii sherehe ziliazimishwa Katika Viwanja vya Ikulu ya nchi Hiyo.






Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga