Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

KAJALA ANASWA NA KIDUME CHINA. KUMBE HAJAFULIA KIHIVYO EEH.


Yap! Staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja ‘K’ anadaiwa kufumwa na mwanaume nchini China huku akisusiwa sherehe ya bethidei yake, Ijumaa Wikienda limeinyaka.

Staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja ‘K’.Kwa mujibu wa kachero wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) aliyepiga kambi Hong Kong, China, mwishoni mwa wiki iliyopita Kajala alionekana na mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina moja la Meddy kwenye pati hiyo ambayo eti inasemekana ilihudhuriwa na watu watatu.
Ilisemekana kwamba Kajala amejibu mapigo kwa kujinyakulia kijana kwa ajili ya kumkosha moyo na kumsafisha na skendo za waume za watu.Ijumaa Wikienda lilipomtafuta Kajala kwa njia ya simu hakuwa hewani na hata alipotumiwa ujumbe kwa WhatsApp hakujihu.hakujib

KAJALA APAKWA VIBAYA INSTA, KAFULIA MBAYA, SOMA HAPA YALIYOMWAGWA KUHUSU YEYE.


Kajala Kwenye News Tena Katika Pita pita zangu Instagram nimekutana na huu Ubuyu kutoka kwa Dougiesmasta akimponda Kajala na Kuandika haya Hapa Chini:
"Hehehehehehehe kama nilivyo sema mbea kazia yake ni kufikisha habari....na habari ndio hiii watu mpoooooooooo kutukanwa sitaki lkn umbe wa mujini ndio huu eeti ndugu yetu billionea kajala wa masanja sasa hiv amekuwa apeche alolo aka alosto kafulia fuli fuli...hatari hapana chezea lakzima utajiuliza kwan bwana Ck yuko WAP...aibu mjin CK ajifungia ndani anamadeni kila kona ya dunia....ck wa kuuza vitu vyake vya ndani inatia huruma billionea kajala wa kutembelea NOAH wakat mbezi ya kimala NOAH dala dala uwiiii....
 
kajala tulikwambia lkn hapa mjini ukifulia hakuna atakae kutaka yuko wapi yule big daddy alokuwa anajifanya anakupenda kumshinda mamako mzazi wote wamekukimbia kajala wewe sio wakujifungia ndani bilionea shauzi kumwaga pesa sasa hiv unazijutia..yani wenzio wananunua magali wewe unauza hatari hii...hiv KAY YAKEE wewe kwann kila mwanaumr utakae kuwa nae lazima aishie jela maskin CK yani kama namuona anavyoenda kunyea debe mpooo CK kazi ndo basi wazee TAKUKURU wamfikisha mahakamani kwa wizi wa pesa za serikali...
 
mungu sio fundi juma tusema ukiwa huna pesa utampa ny... mungu wako wewe ndio wawote kajala ulifurahi Sana Wema alipo pokonywa gali kipo WAP huyo bwana alokuwa anakutia jeuri sasa hiv kabaki yeye na tumbo lake...KAY VIP China mbona hatuoni tena safari zimeingia mchanga au hahahahahaha jamn jmn msipende kuchezea pesa zikiisha utaanza kukumbuka unao wadai wote
NAENDELEA UMBUYU MREFU" By Dougiesmasta

WENGINE HATUISHI KWA KUTEGEMEA WANAUME "KAJALA"


MSANII Kajala ametamka kwamba siyo kila mwanamke mwenye fedha anatoa kwa wanaume, wengine wana madili mjini kutokana na kuja kitambo.

“Sidhani kama kuna mtu anayenifahamu vizuri, hamfahamu kuwa mimi ni mjanja na nimezaliwa mjini kitambo, katika suala la kusaka mkwanja hakuna mwenye cha kuniambia, hivyo kila nilichonacho ni kwa jasho langu na kutumia akili siyo za kupewa kama zawadi, ”anasema Kajala ambaye amekuwa akihusishwa na ugomvi wa kimasilahi na msanii wa filamu Wema Sepetu.

“Hata ukiona nimeandikwa vibaya, nimesemwa vibaya, nimetishwa, usifikiri nakosa usingizi au naahirisha safari ya China au Dubai, hapana nakwenda kwa sababu nafahamu wanaosema ni madebe matupu hawaachi kupiga kelele.”

“Kuna watu wapo kati kati yangu na marafiki zangu, lakini mimi ninawapenda na kuwaheshimu wote, kwani naamini wana mchango mkubwa kwangu hata kama wao hawafahamu hilo,” anasema Kajala , mrembo kutoka Mkoani Mwanza aliyejaaliwa umbo la kuvutia.

WOLPER AMSALITI KAJALA KWA "WEMA SEPETU"



UNAFIKI 100%! Wakati kila mtu akiamini kwamba staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe ni shosti wa Kajala Masanja ‘Kay’, ameibua mshangao baada ya kunaswa akikumbatiana na Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ ambaye kwa sasa haziivi na Kay.
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper akishoo love na Wema Sepetu.
TUJIUNGE KWENYE BETHIDEI
Tukio hilo lililoibua maswali mengi yasiyokuwa na majibu ya harakaharaka lilijiri hivi karibuni katika bethidei ya shosti wa damu wa Wema, Aunty Ezekiel Grayson ambayo ilifanyika kwenye Mgahawa wa Rodizio, Masaki jijini Dar.
WAKUMBATIANA
Huku paparazi wetu akishuhudia na kuwafotoa picha, Wema alipoingia tu ukumbini humo, alimkuta Wolper akila raha zake ambapo alimkimbilia kisha akamkumbatia kwa dakika kadhaa huku wakimwagiana mabusu kuonesha wamemaliza tofauti zao na kwamba walikuwa ‘wamemisiana’.
Wakati wamekumbatiana na kupigana mabusu walikuwa wakinong’onezana mambo yao ambapo walipomaliza waliachia vicheko vilivyosikika ukumbi mzima ndipo minong’ono ikaanza.
WATAALAM WA UBUYU 
Kitendo cha Wema kutumia dakika kadhaa kukumbatiana na Wolper, kilitafsiriwa na wataalam au wafuatiliaji wa mambo ya watu (ubuyu) kuwa ni usaliti mzito kwani Wolper ni Timu Kajala ambaye ni hasimu mkubwa wa Wema.
Wema Sepetu akimhagi Jacqueline Wolper.
“Mh! Mwenzangu makubwa, huyu Wolper si ni Timu Kajala? Inakuwaje anatoa ushirikiano wa asilimia mia moja kwa adui wa Kajala? Hapa kuna tatizo, unafiki kwa mastaa kamwe hauwezi kuisha,” alisikika mtoa ubuyu mmoja aliyeomba hifadhi ya jina gazetini.
AKUMBUSHA VITA YAO
Kama hiyo haitoshi, mtoa ubuyu huyo alikwenda mbali zaidi kwa kusema, ukiachilia mbali Wolper kuwa karibu na Kajala lakini hata yeye (Wolper) alikuwa kwenye vita nzito na Wema kwa kudaiwa ‘kushea’ naye penzi la msanii Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
“Wolper jamani mnafiki...si ndiyo huyuhuyu aliwahi kuingia kwenye vita nzito na Wema baada ya kudaiwa kuwa anadondoka dhambini na kipenzi cha Madam, Diamond? Yaani huu ni unafiki asilimia mia,” alisema mtoa ubuyu huyo.
TIMU KAJALA WAJA JUU
Baada ya Timu Kajala kusikia kwamba Wolper ‘ali-spendi’ vya kutosha na Madam kwenye bethidei hiyo, walikuja juu kisha wakamtolea uvivu na kuanza kumshambulia katika mitandao ya kijamii na kudai hafai kuwa timu yao.
Huku wakati huo huo... Jacqueline Wolper akishea urojo sahani moja na Kajala Masanja ‘Kay’.
“Wolper msaliti, ataendaje kwenye sherehe ya mpinzani wetu? Tena kama hiyo haitoshi, yeye anakumbatiana na Madam ambaye kwetu sisi hatusaidii lolote,” alisema mmoja wa Timu Kajala.
KUMBUKUMBU IPOJE?
Kabla ya siku hiyo, Wolper na Wema hawakuwahi kuwa na uhusiano mzuri na kila sehemu ambayo utakumta Wolper, kamwe huwezi kuona Wema ametia maguu.
WOLPER ANASEMAJE?
Baada ya paparazi wetu kushuhudia kitendo hicho ukumbini, alimfuata Wolper na kumuuliza ni kitu gani kilichowasababisha wapatane na kuoneshana ‘mahaba niue’ wakati nyuma ya pazia wana bifu? Msikie alichojibu:
“Ujue watu wengi sana wamekuwa wakidhani mimi na Wema tuna bifu, sijui kwa kuwa mimi nina ukaribu na Kajala au kwa kuwa hatujawahi kuwa pamoja, lakini ukweli mimi na Wema siyo waongeaji sana japokuwa huwa nikiweka picha au chochote kwenye Instagram, Wema huwa ana-like na mimi huwa na-like vitu vyake hivyo sidhani kama nilikuwa na tatizo naye sana,” alisema Wolper.
TUJIKUMBUSHE
Urafiki wa mastaa huwa mara nyingi haudumu, Wema ambaye hivi sasa shosti wake mkubwa ni Aunty, kabla aliwahi kuwa na urafiki na Snura Mushi, Jamilah wa Temba, Kajala na wote hao akawamwaga.

BINTI WA KAJALA AWA GUMZO "MLIMANI CITY"


SEXY lady wa filamu Bongo, Kajala Masanja hivi karibuni aligeuka gumzo yeye na mwanaye walipoenda kufanya ‘shopping’ Mlimani City ambapo watu walikuwa wakiwakodolea macho kwa jinsi alivyolingana na mtoto wake.
Sexy lady wa filamu Bongo, Kajala Masanja akiwa na mwanaye Paula.
Kajala alitinga eneo hilo na mtoto wake huyo aitwaye  Paula ambapo awali walienda kupata chakula katika mgahawa wa SamakiSamaki  na kisha waliingia ndani kwa ajili ya kufanya manunuzi mengine.
“Kwa kweli Kajala amekuza maana yeye na mtoto wake wamelingana sasa na mara nyingi kwa sasa hivi wanaongozana huku wakionekana kuwa na furaha wakati wote,” alisikika mtu mmoja akizungumza.
Watoto wengine wakimkodolea binti wa kajala, Paula maeneo ya Mlimani City.
Kajala alipozungumza na  mwandishi wetu alisema kuwa hakuna kitu kinachompa furaha kama mtoto wake huyo na anapoongozana naye anazidi kufurahi zaidi.
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga