Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

» » » » WENGINE HATUISHI KWA KUTEGEMEA WANAUME "KAJALA"


MSANII Kajala ametamka kwamba siyo kila mwanamke mwenye fedha anatoa kwa wanaume, wengine wana madili mjini kutokana na kuja kitambo.

“Sidhani kama kuna mtu anayenifahamu vizuri, hamfahamu kuwa mimi ni mjanja na nimezaliwa mjini kitambo, katika suala la kusaka mkwanja hakuna mwenye cha kuniambia, hivyo kila nilichonacho ni kwa jasho langu na kutumia akili siyo za kupewa kama zawadi, ”anasema Kajala ambaye amekuwa akihusishwa na ugomvi wa kimasilahi na msanii wa filamu Wema Sepetu.

“Hata ukiona nimeandikwa vibaya, nimesemwa vibaya, nimetishwa, usifikiri nakosa usingizi au naahirisha safari ya China au Dubai, hapana nakwenda kwa sababu nafahamu wanaosema ni madebe matupu hawaachi kupiga kelele.”

“Kuna watu wapo kati kati yangu na marafiki zangu, lakini mimi ninawapenda na kuwaheshimu wote, kwani naamini wana mchango mkubwa kwangu hata kama wao hawafahamu hilo,” anasema Kajala , mrembo kutoka Mkoani Mwanza aliyejaaliwa umbo la kuvutia.

About Unknown

Habari karibu katika Blog hii, Tafadhali Like Page Yetu na Toa Maoni yako kuhusiana na kile unachokiona humu.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga