Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

CCM YAWATEKA WASANII WA BONGO MOVIES, MAMIA WAJIUNGA RASMI.


Chama cha Mapinduzi (CCM) kimefanikiwa kupata wanachama wapya ambao ni wasanii wa tasnia mbalimbali, miongoni mwao ni Uwoya, Johari, Banana, JB na Mrisho Mpoto.

Chanzo: Jamii FORUMS

SNURA ALIA NA WABAYA WAKE, WANAOTAMANI AANGUKE.


STAA aliyeliteka soko la mduara kwa kibao chake cha Majanga, Snura Mushi amesema watu wenye chuki na yeye wamepanga njama za kumshusha kwenye chati kutokana na maendeleo yake.
Snura Mushi.
Akipiga stori na paparazi wetu juzi, Snura alisema: “Nashangaa sana ninapofanya jambo zuri halafu watu wanaligeuza kuwa baya ili nichafuke jina na kunipunguzia mvuto kwa mashabiki wangu.”
Chanzo cha yote ni baada ya mwanadada huyo kupiga shoo kwenye Ukumbi wa Buliyaga, Temeke, Dar siku chache zilizopita, kundi la watu wasiojulikana walianza kueneza taarifa kuwa alifanya vibaya na mashabiki wakamtaka ashuke jukwaani jambo ambalo alisema halikuwa na ukweli wowote.

"NINGEMKOSA H BABA MAISHANI MWANGU NINGEYUMBA" FLORA


UA la Bongo Movies, Flora Mvungi amefunguka kuwa anashukuru Mungu kumpata mume mwema, Hamisi Baba ‘H.Baba’ kwani vinginevyo angeyumba kimaisha.
Flora Mvungi na mumewe H. Baba.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Flora alisema H. Baba ni mwanaume anayestahili sifa zote hivyo endapo angekutana na mwanaume mwingine basi angeyaona mapenzi machungu.
“Mungu hakukosea kuniletea H. Baba, nampenda sana kwani ni mtu anayenijali mimi na mtoto wetu Tanzanite yaani sijui kitu gani ambacho nakikosa kwake, bila huyu maisha yangeyumba,” alisema Flora.

RAYUU BADO ANATAMANI KUTEMBEA NA MUME WA MTU, ASEMA HAWEZI KUJIZUIA.


MSANII kinda kwenye tasnia ya filamu Bongo, Rahma Bagenzi ‘Rayuu’ amesema kuwa, kamwe hatokoma kutembea na waume za watu kwa kuwa sheria ya dini yake ya Kiislamu inamruhusu kuolewa na mume wa mtu.
Rahma Bagenzi ‘Rayuu’.
Akipiga stori na paparazi wetu, Rayuu alisema kipindi cha nyuma aliwahi kutoka kimapenzi na mume wa mtu (hakumtaja jina) na kufikia hatua ya kufikishwa polisi na mwenye mke lakini haimaanishi kuwa hatatembea tena na mume wa mtu.
“Nikila kiapo cha kutotembea na waume za watu nitakuwa naongopa, kwanza dini yetu imeruhusu ndoa za uke wenza huenda  Mungu kaniandikia niolewe ndoa ya aina hiyo sina uwezo wa kupingana naye,” alisema Rayuu.

GPL.

DR CHENI APANIA KUIRUDISHA KAOLE SANAA GROUP.


MWENYEKITI Msaidizi wa Bongo Movie Unity, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ amesema amekumbuka na kutamani kurudisha Kundi la Sanaa ya Maigizo la Kaole ‘Kaole Sanaa Group’ liwe na nguvu kama zamani.
Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’.
Dk. Cheni alisema japo kundi hilo limeonekana kupoteza mvuto wake wa awali, lakini anaamini wasanii wengi wanaofanya vizuri kwenye tasnia ya filamu kwa sasa wametoka katika kundi hilo maarufu.
Hata hivyo, pamoja na kupotea kwa kundi hilo, Dk. Cheni anatamani sana kulirejesha kwenye ulingo wa sanaa na kwamba kuna mikakati anayoiandaa ili kukamilisha azimia hiyo.
“Naitamani Kaole ya zamani, nahisi kama kuna vionjo vinakosekana siku hizi. Wasanii wengi wenye majina makubwa kwa sasa wametoka kwenye kundi hilo, lakini nitajitahidi kulirudisha, naamini nitafanikiwa,” alisema Dk. Cheni.

BAADA YA KUJIINGIZA KIAINA NA SIASA, WANA BONGO MOVIES WAMTAKA STEVE NYERERE AJIUZULU.


Hali si shwari katika klabu ya wasanii wa filamu za Kibongo, Bongo Movie Unity ikidaiwa kuwa baadhi ya ‘memba’ wake wanashinikiza mwenyekiti wake, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ajiuzulu.
Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Habari zilizoifikia Stori Extra wikiendi iliyopita zilidai kuwa, baadhi ya wasanii wa klabu hiyo akiwemo mwenyekiti huyo walilamba mshiko kutoka kwa mwanasiasa mmoja wa CCM mkoani Mbeya ili wamfanyie kampeni katika uchaguzi ujao jambo ambalo wenzao walilipinga vikali kwa kuwa wao hawajihusishi na siasa bali wasanii na jamii.
Alipotafutwa Steve kujibu tuhuma hizo hakupatikana lakini katibu wake, William Mtitu alikiri kuwepo kwa ishu hiyo.
GPL.

SHERIA YA KUWANYONYESHA WATOTO KWA MIAKA MIWILI YAPISHWA HUKO UARABUNI.


Wanawake wa Umoja wa nchi za Kiarabu wanatakiwa kuwanyonyesha watoto zao kwa kipidi cha miaka miwili, sheria mpya ya kutetea haki za watoto ambayo imeanza kutumika rasmi mwezi huu imeeleza.

Sehemu ya sheria hiyo mpya, inawataka wamama kuwanyoyesha watoto zao kwa miaka miwili kamili au waume zao wataweza kuwashtaki kama watashindwa kufanya hivyo.
DC Blog.

JUSTIN BIEBER AINGIA KATTIKA SKENDO TENA, ANASWA LIVE AKILAMBA CHUCHU ZA K@HABA.


Miaka 19 aliyonayo inampeleka puta na kuzidi kuashiria ule usemi usemao, ujani ni maji ya moto, mwanamuziki  mwenye mafanikio, raia wa Canada, Justine Bieber, juzi juzi alifanya boonge la party na kuwaalika miongoni mwa washkaj zake, mbali na hiyo ali mualika K@haba mmoja kwa ajili ya kucheza akiwa mtupu huku akivalia maziwa makubwa ya juu.

Katika kunegesha shughuli nzima, Bieber na Mshkaji wake Khalil, walipeana chuchu moja moja kunyonya kama wanavyoonekana pichani.

BAADA YA KUANZISHA KANISA LAKE, MAAJABU YAANZA, SURA YA KANYE WEST YAOTA MGUUNI KWA MREMBO HUYU


Baada ya Kanye West kufunguka na kuanzisha Kanisa lake huku akitaka kuabudiwa yeye, kumeibuka mambo ya ajabu huku kubwa ni hili la sura ya Kanye West kutokea katika mguu wa mwanadada mrembo huyu. angalia picha zaidi hapa:-

.

AFANDE SELE AIFAGILIA BANGI KAMA OBAMA.


Afande Sele ameungana na Rais wa Marekani Barack Obama katika kuunga mkono kauli yake ya kwamba bangi ni salama kuliko pombe kwa afya ya binadamu.

Akiongea na kipindi cha Milazo XP kinachorushwa na TBC fm, Afande Selle, mbali na kuunga mkono pia alizungumzia umuhimu wa bangi kama zao linaloweza pia kuwa na manufaa kwa uchumi wa nchi kama litatumiwa kwa usahihi.

Sikiliza mahojiano hayo hapa....

Fuata link hii kusikiliza:- http://old.hulkshare.com/tjcqooymf56o

DC Blog.

HATIMAYE BEYONCE KUANZA KUSOMWA KAMA SOMO KATIKA KOZI ZA CHUO.


Queen Bee ameungana na watu wengine mashuhuri kama Oprah na mume wake Jay Z, (ambaye ana kozi sociology iliyopewa jina badala yake kwenye Chuo cha Georgetown), ambayo yanafundishwa kwenye vyuo. Kozi hiyo inaitwa Politicizing Beyonce na itakuwa inafundishwa na Chuo cha Rutgers cha New Jersey.

Kitengo cha Masomo ya Jinsia ya Wanawake kitakuwa kikifundisha juu ya jamii na utamaduni ya muimbaji huyo kimuziki na mfano wake.

DC Blog

PATA MUDA KUANGALIA PICHA ZA MVULANA WA KIPINDI HICHO ALIVYOJIBADILI NA KUWA MSICHANA HUYU PICHANI, HUWEZI AMINI.


Hii ni zaidi  ya laana, nami sina la kusema, tumwachie Mola atahukuma, maana huyu zamani alikuwa kijana handsome boy wa maana, leo hii kajigeuza na kuwa msichana kwa matakwa yake, angalia picha zaidi hapo chini.

 



































Eti ana Boy Friend kabisaa.




BABA AMUAUA MWANAE WA MIEZI 6 KWA KUMPIGA NA CHUPA YA BIA KICHWANI.

Masikini wa Mungu! Baba aliyetajwa jina moja la Shaban (25), mkazi wa Kimara-Suka, Dar anadaiwa kuhusika katika mauaji ya mtoto wake asiye na hatia, Salma Shaban (miezi sita) kwa kumpiga na chupa ya bia kichwani na kusababisha mshipa mkubwa wa damu kukatika kichwani.
Mtoto aliyeuwawa na Baba yake, Shaban.
Akilisimulia Risasi Jumamosi mkasa huo wa kuumiza moyo, mama mzazi wa mtoto huyo, Matlida Amon alieleza kuwa tukio hilo lilijiri maeneo hayo hivi karibuni majira ya 5:00 asubuhi.
Mama huyo alimtaja kwa machungu mzazi mwenzake huyo kuhusika na tukio hilo.
Mama mzazi wa mtoto huyo, Matlida Amon.
Alisema kuwa mumewe huyo wa ndoa alimuomba aende kumchajia simu barabarani ambapo alimuacha mdogo wake wa kike mwenye umri wa miaka 13 na mtoto akiwa anacheza kitandani.
Alisimulia kuwa aliporudi nyumbani alishangaa kumkuta mdogo wake akilia nje ya nyumba yao.
Matlida alisema kuwa alipomuuliza mdogo wake kwa nini alikuwa akiangua kilio, akamwambia kwamba shemeji yake alikuwa akimwambia kuwa anataka kufanya naye mapenzi.
Baba wa mtoto Shaban (25), mkazi wa Kimara-Suka.
Alisema mdogo wake alimwambia kuwa alimsukumiza kitandani akitaka kumbaka ndipo akapiga kelele na kufanikiwa kumchomoka na kukimbilia nje.
Mama wa mtoto huyo aliendelea kusimulia kwamba alipoingia ndani alianza kumlaani mumewe huyo kwa kitendo alichotaka kukifanya kwa mdogo wake ambapo aliishia kuomba msamaha lakini alimwambia ni bora amuombe mdogo wake (shemeji) na siyo yeye.
Matilda alisema kuwa baada ya kumwambia hivyo, yeye alianza kukusanya nguo za mdogo wake ampe ili aende nyumbani kwao ndipo mumewe huyo alipochukua kisu alichokiweka pembeni ya godoro na kutaka kumchoma nacho yeye.
Hata hivyo, Mungu mkubwa kwani Matilda alisema kuwa alifanikiwa kukidaka na kwa vile kilikuwa kibovu mwanaume alibaki na mpini yeye akabaki na kisu bila mpini.
Alisema alikitupa kisu hicho kupitia dirishani ambapo alipogeuka mumewe, alimzibua kibao kikali usoni kisha akachukua chupa ya bia iliyokuwa tupu ndani na kwenda moja kwa moja kwa mtoto aliyekuwa akicheza kitandani na kumpiga nayo kichwani huku akisema: “Bora tukose wote.”
Matilda aliendelea kusimulia huku akilia kuwa baada ya kufanya kitendo hicho baba huyo alikimbia huku yeye akimkimbilia mtoto aliyekuwa akitapatapa kitandani.
Dakika chache baadaye mtoto alizimia hivyo baadhi ya majirani walimkimbiza katika Hospitali ya Boch iliyopo Kimara-Suka, Dar ambapo alipatiwa huduma ya kwanza kisha wakampiga X-Ray na kugundua kuna mshipa mkubwa wa fahamu kichwani ulikuwa umekatika.
Baada ya hapo alikimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar. Alipofikishwa aliingizwa kwenye chumba cha upasuaji ili kuokoa maisha yake lakini ilishindikana kwani alifariki dunia.



Baada ya kupata taarifa hizo, ndugu pamoja na mama wa mtoto huyo walikwenda katika Kituo cha Polisi cha Mbezi Kwayusuf na kuandikisha taarifa kisha wakapatiwa jalada la kesi namba KMR/RB/1017/2014 na KMR /735/2014- MAUAJI ambapo mtuhumiwa anasakwa na polisi ili kufikishwa kwenye mkono wa sheria.
GPL.
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga