-->
Kama kawaidayao, Wachina wafungua jengo hilo baada ya kukamilia ujenzi wake, Jengo hilo kubwa kuliko yote duniani lina Urefu wa Ghorofa 18 Tu, Kama letu la Benjamin Mkapa Pension Towers uongeze na ghorofa 3 hivi juu.
Ukubwa wa jengo hili ni kutokana na upana wake ambao unafikia Kilomita za Mraba Milioni 1.2, Jengo hili lipo huko Chengdu, kwa ukubwa wake zinaweza kuingia Pentagon 3 za wamarekani, Miji minne(4) ya Vatican na zaidi ya nyumba 20 za Sydney Opera.
Jengo hilo lina maduka kadhaa ya kufanyia shopping za mahitaji mbali mbali, na Hotel kubwa za hadhi ya Nyota 5 mbili, kila moja ikiwa na vyumba 1,000.
Mbali na hayo jengo hilo lina mandhari nzuri kwa nje kuanzia pools na bustani huku kukiwekwa mitambo maalum ya jua la kutengeneza ili kutoa kivutio katika hizo pools. Kwa hesabu za sasa jengo hilo ni kubwa kuliko viwanja 329 vya mpira wa miguu vikiwekwa pamoja.
Uzinduzi rasmi wa jengo hilo unatarajia kufanywa mnamo August 22.