Siku chache zilizopita Hospitali ya St Ives ya Huko Lagos ilipatwa na furaha isiyokuwa kifani baada ya mama mmoja alikuwa na umri wa miaka 53 alipojifungua mapacha wawili wa kiume. Mwanamke huyo alijifungua watoto hao baada ya kusubiri kwa zaidi ya miaka 20 bila kuwa na mtoto.
Baada ya kukaa mika yote hiyo bila mtoto, aliamua kubadilisha njia ya kupata ujauzito na kujaribu Invitro Fertilisation (IVF), njia ambayo hufanywa kwa yai la uzazi la mwanamke kupevushwa nje ya mwili wake na manii kila muda unapofika na kisha huwekwa katika mashine maalum kwa takribani siku nne hadi tano na kisha hurudishwa katika mwili wa mwanamke.