Hali ya Usalama ya Raia wa Uingereza wanaotalii huko Uturuki inazidi kuwa mbaya baada ya Raia mwingine Kushambuliwa kwa kupigwa na chupa kichwani maeneo ya fukwe za mji wa Marmaris, kiasi cha kumfanya avuje damu sana na kama si kuwahi kupatiwa msaada wa kitabibu angepoteza maisha.
Hili ni tukio la pili baada ya tukio la wiki iliyopita ambalo kijana mwingine wa Uingereza Dayne Ward, 17, alishambuliwa kwa kisu halafu kuvuliwa nguo zote ma kutupwa ili afe.