Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

» » KUTANA NA KIJANA ANAEISHI KWA KULA MIFUKO YA PLASTIKI, AMEANZA TABIA HIYO TANGUA AKIWA NA MIAKA 7, SASA ANA MIAKA 23.


Oakland.Kijana mwenye umri wa miaka 23 amejikuta katika wakati mgumu, baada ya kuathiriwa na tabia ya kula mifuko na bidhaa za plastiki.
Kijana huyo, Robert kutoka huko Oakland, Tennessee nchini Marekani alianza tabia hiyo kama mzaha akiwa na umri wa miaka saba tu, ambapo alipendelea zaidi plastiki za rangi ya bluu ambazo kwa mtazamo wake alikuwa akiona rangi hiyo ina utamu.
Kadiri miaka ilivyozidi kuongezeka, tabia hiyo ilimwathiri na hata kujikuta akilazimika kutumia mbinu za ziada kuipata, ikibidi kwa kuiba kwenye maduka makubwa au kwenye maduka ya mitaani.
Si hivyo tu, mara nyingine huchukua hatua ya kuiba mifuko ambayo huhifadhiwa matunda kwa ajili ya maonyesho kwenye maduka na kuyamwaga kisha kutokomea na mifuko hiyo.
Tangu alipoanza tabia hiyo, imeelezwa kwamba tayari ameshatafuna zaidi ya mifuko 60,000 ya plastiki ambayo kwa wingi wake inaweza kujaza uwanja wa kuchezea mpira wa miguu.
Kwa mujibu wa maelezo yake, huanza siku yake kwa kula mfuko wa kwanza kama kifungua kinywa na hupendelea zaidi mifuko ya rangi ya bluu ambayo hutumiwa kufunga magazeti.
Alieleza kwamba muda mwingine hulazimika kuanza kurandaranda kwenye nyumba za jirani akitafuta mifuko hiyo ambayo wengi wa majirani huitupa ovyo baada ya kufungua na kuchukua magazeti yao ili kukidhi haja yake.
Robert anaamini kwamba mifuko yenye rangi nyingine tofauti na rangi ya bluu pia ina ladha tofauti, hivyo wakati wa majadiliano yake na kituo cha TLC katika kipindi chake cha Tabia Yangu ya Ajabu alisema anaona bluu ni tamu zaidi.
Mara nyingine hulazimika kukaa hadi siku moja na nusu bila kula chakula iwapo atapata dozi ya kutosha ya mifuko hiyo, ambapo baada ya kujisaidia hali yake hurejea kama kawaida na kuendelea na shughuli zake.
Kitendo hicho kimewashangaza wengi kwa kuwa hata baadhi ya majirani hawakuwahi kujua kwamba kwa miaka yote alikuwepo kijana ambaye alikuwa akiwasaidia kupunguza taka za mifuko ya plastiki majumbani kwao.
Hata hivyo, mchumba wake, Ashley alisema amekuwa akisumbuliwa sana na tabia hiyo ya Robert na amekuwa akijaribu kufanya kila juhudi ili aachane nayo kabla ya ndoa yao inayotarajiwa kufungwa miezi sita ijayo.
Not happy: Fiancee Ashley is concerned over his addiction and wants him to stop consuming so many
Jambo la kushangaza ni kwamba, japokuwa kitaalamu ulaji wa plastiki kwa binadamu husababisha kuziba kwa utumbo na kuharibu ini, vipimo alivyochukuliwa Robert vinaonyesha kwamba hana athari zozote katika maeneo hayo.
Katika mtiririko wa matukio yake, Ashley alisema aliudhika zaidi siku walipokwenda kutafuta keki kwa ajili ya harusi yao, ambapo Robert alipotakiwa kuonja alishindwa akisema kwamba ameshiba kupita kiasi kutokana na plastiki alizokula.
Muda mfupi baadaye alilalamika kwamba ana maumivu ya tumbo na baada ya kushauriwa kwa muda ndipo alipokubali kwenda kumwona daktari kwa ajili ya vipimo.
Check-up: Even though eating plastic can cause liver damage and intestinal blockages, Robert's tests come back OK but he is going to try and cut down
Japokuwa Ashley amefahamu kuathirika huko kwa mchumba wake tangu walopoanza uhusiano zaidi ya miaka miwili iliyopita, anasema aliona ni jambo linalohitaji ukaribu na msaada zaidi ili kumwepusha na tabia hiyo.
Kwa ajili ya upendo na map#nzi yake kwa Ashley, Robert kwa sasa amemwahidi mchumba wake huyo kwamba atafanya kila linalowezekana kuacha tabia hiyo ili kuwezesha ndoa yao iwe ya amani mara wakati utakapofika.
Mwananchi/Daily Mail.

About Unknown

Habari karibu katika Blog hii, Tafadhali Like Page Yetu na Toa Maoni yako kuhusiana na kile unachokiona humu.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga