BAADA YA MAJAMBAZI KUMUUA NA KUKATA "NYETI" DEREVA WA MALORI, WENZAO WAFUNGA BARABARA HUKO MWANZA.
MADEREVA wa malori wameamua kuziba barabara ya Mwanza - Dar es Salaam kuanzia leo asubuhi baada ya majambazi kumuua mwenzao, kumkata nyeti na kumtoboa macho jana.
Tukio hilo limesababisha foleni kubwa iliyoanzia Igunga mpaka Nzega huku kukiwa hakuna gari lolote linalovuka kutoka Dar kwenda Mwanza au Mwanza kwenda Dar.
Abiria waliokuwa wanasafiri waliamua kutulia wakiwa hawajui nini hatma yao.