Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

ZARI NA DAIMOND MAMBO NI MOTOMOTO, CHEKI MAPOKEZI YA DAIMOND KAMPALA JANA...


Staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' akiwa na mfanyabiashara mrembo na muimbaji wa Uganda, Zarinah Hassan 'Zari'  au 'The Boss Lady' baada ya kuwasili Uganda jana.
Diamond Platnumz akiwa na Zari the Boss Lady wakiondoka Uwanja wa Ndege wa…
Staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' akiwa na mfanyabiashara mrembo na muimbaji wa Uganda, Zarinah Hassan 'Zari'  au 'The Boss Lady' baada ya kuwasili Uganda jana.
Diamond Platnumz akiwa na Zari the Boss Lady wakiondoka Uwanja wa Ndege wa Uganda.
Diamond Platnumz akiwa na Zari the Boss Lady kwenye pozi.
Diamond Platnumz na Zari wakipigwa picha na wanahabari.
Diamond Platnumz na Zari wakijiandaa kuongea na wanahabari jana.
Staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani).
STAA wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' ameondoka Tanzania jana mchana na kuelekea Uganda kwaajili ya hafla ya Zarinah Hassan 'Zari'  au 'The Boss Lady inayoitwa ZariAllWhiteCirocParty inayofanyika Kampala.

TIBAIJUKA AGOMA KUJIUZULU, ADAI YEYE HANA FASHION HIYO.


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka, akiongea na wanahabari hivi punde ndani ya Hyatt Regency Hotel Dar es Salaam amesema haoni sababu ya kujiuzulu kutokana na sakata la akaunti ya Escrow.
Aongeza kuwa watu wanaona suala la kujiuzulu kama fasheni ila yeye hayupo katika fasheni hiyo.

AISHA MADINDA KUZIKWA KESHO DAR



ALIYEKUWA mnenguaji na mwimbaji wa Bendi ya Twanga Pepeta, Aisha Madinda aliyefariki jana asubuhi, atazikwa kesho mchana badala ya leo kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali.
Mtoto wa kwanza marehemu, Feisal amesema kuwa polisi wamesema ni lazima mwili wa mama yake ufanyiwe upasuaji (postmortem) ili kujua chanzo cha kifo chake.

Awali ndugu wa marehemu walisema hawahitaji Asha Madinda afanyiwe upasuaji, lakini baada ya polisi kutembelea eneo la tukio la kifo chake huko Mabibo, wamesema ni lazima upasuaji ufanyike.
Feisal amesema upasuaji unatarajiwa kufanyika leo mchana hali inayowalazimisha kubadili ratiba ya mazishi. Aisha Madinda sasa atazikwa kesho mchana baada ya sala ya Ijumaa.

WANAJESHI 100 WAHUKMIWA KIFO KWA KUSHINDWA NA BOKO HARAM



Mahakama ya Kijeshi nchini Nigeria imewahukumu adhabu ya vifo wanajeshi wake 54 waliokataa kupambana na wapiganaji wa Kundi la Boko Haram.

Wanajeshi hao walikutwa na hatia ya uasi, kushambulia na uoga. Wanajeshi hao wanashutumiwa kukataa kupigana kurudisha miji mitatu iliyokuwa ikishikiliwa na Boko Haram mwezi Agosti.
Mwanasheria wa wanajeshi hao amesema wamehukumiwa vifo kwa kupigwa risasi na kikosi maalum huku wanajeshi wengine watano wakiachiwa.

Vikosi vya Kijeshi vya Nigeria vimedai kuzidiwa silaha na Boko Haram, kwa kuwa hawapatiwi silaha za kutosha kupambana na wanamgambo hao.
Boko Haram wanapambana kuunda himaya ya kiislamu kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
CHANZO: BBC

WASANII WA KENYA WANYANYASIKA KATIKA SHOW YA DAIMOND PLATINUMZ NYUMBANI


Kunyanyaswa kwa wasanii wa Kenya, kumemfanya Diamond na waandaji wa show yake ya Mombasa weekend iliyopita kutupiwa lawama na wapenzi wa muziki nchini humo.

Mtandao wa Standard Media wa Kenya, umeandika kuwa kwenye show hiyo iliyohudhuriwa na watu kibao, Diamond alitaka wasanii wengine wote waliokuwa watumbuize kwenye show hiyo na waliokuwa wamepangiwa kukaa naye kwenye VIP lounge, wakiwemo Susumila na Nyota Ndogo waondelewe.

   Ilidaiwa pia kuwa Susumila na Nyota Ndogo walinyimwa maji ya kunywa na kwamba waliambiwa wanywe maji ya bomba kwakuwa maji ya kwenye chupa yalikuwa kwaajili ya Diamond peke yake.

Tukio hilo liliwafanya wasanii wa Mombasa waungane kuwalaani waandaji wa show hiyo ambapo VJ Delph alikataa kucheza muziki.

  “Kama hili likiendelea, wapenzi wa muziki wa Mombasa watagomea show za Diamond mbeleni. Ni fedheha kwa wasanii wetu kutendewa hivyo nyumbani,” alisema Hassan Faisal wa Coastal Films.

LULU NA MAONI YAKE KUHUSIANA NA FASHION


Kwa mtazamo wake Msanii Lulu Michael amedai kuna tofauti kati ya style na Fashio, kwake ameona Fashion ni kile tunachonunua na Style ni Kile tunachovaa. nahisi hapa kachemka sema kwa kuwa ni staa tuimezee.

ZARI NDO FAVOURATE JUICE YA DIAMOND PLATINUMZ


Baada ya Kukataa ukweli kwa muda mrefu, huku akidai hana mahusiano ya kimapenz na mrembo tajiri kutoka Uganda Zarina Hassan "Zari". Diamond sasa anaonekana kunogewa na penz la mrembo Huyo na kuthibitisha kuwa Zari ndo Juice Yake anayoipenda.

Diamond Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameposti Picha ya mrembo Zari na Kuandika maneno Haya. "My Favourite Juice." Water melon. Akimaanisha kuw Mrembo zari ndiye anaempa raha na mtamu kama juice.Lol acha project iendelee

ALICHOKISEMA LULU KUHUSIANA NA MISS TANZANIA KUSHINDA TAJI LA MISS WORLD


MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael 'Lulu' amendika katika Instagram kuwa mshiriki wa Tanzania kwenye Miss World, Happiness Watimanywa akishinda atabadilisha jina na kuitwa…
Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael 'Lulu'.

LULU NI RAFIKI TU...."IDRIS"



KWA mara ya kwanza baada ya kutua Bongo, Mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshort (2014), Idris Sultan amemfungukia mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ na kudai ni rafiki yake wa karibu.

Mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Sultan.
Kabla mshindi huyo hajakanyaga Bongo, Lulu alishambuliwa mitandaoni baada ya kujinadi kuwa na urafiki wa karibu na Idris lakini kwa kauli hiyo, imeonesha dhahiri wawili hao ni marafiki wa kweli tofauti na mitazamo ya wadau mitandaoni.
Mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’.
“Lulu ni rafiki yangu wa muda mrefu, hakuna kingine zaidi ya urafiki. Tutaendelea kuwa marafiki hata baada ya ushindi huu,” alisema Idris, juzi alipokuwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam (The Kilimanjaro).

KARATAZI ZA KUPIGIA KURA ZANASWA ZIKITOLEWA COPY MTAANI


Dar es Salaam. Wakati Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ukitarajiwa kufanyika kesho nchi nzima, wafuasi wa (Chadema) na Jeshi la Polisi, wamekamata karatasi zinazodaiwa za kupigia kura kwenye uchaguzi huo za Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, zikirudufiwa jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Katibu wa Chadema Jimbo la Ubungo, Justine Mollel, tukio hilo lilitokea juzi saa 12 jioni wakati mwanachama wa chama hicho alipokwenda katika duka la vifaa vya shule na ofisini saa 8 mchana kwa lengo la kurudufu karatasi za chama hicho lakini aliambiwa arudi saa 12 jioni.
Gazeti hili lilifanikiwa kuiona moja ya nakala hizo kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo ikiwa na nembo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, ikiwa na nafasi ya kupigia kura kwa wagombea wa CCM na Chadema.
Habari zaidi zinaeleza kuwa tayari zaidi ya nakala milioni moja zilisharudufiwa, huku zikiwa zimewekwa alama ya ndiyo kwa mmoja wa wagombea wa vyama hivyo.
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alisema: “Uchunguzi bado unaendelea kwani waliokuwa wanarudufu walijitambulisha kuwa ni wasimamizi wa uchaguzi, hivyo tunaendelea na uchunguzi na hakuna mtu tunayemshikilia.”
Aliongeza: “Nimemwagiza OCD (Mkuu wa Polisi wa Wilaya) kuwasiliana na Tamisemi (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) ili kujua hizo karatasi ni kweli zilitakiwa kutengenezwa hapo au la... Kama ni hapo mambo yaishie palepale na kama siyo halali basi hatua zichukuliwe kwa wahusika.”
Mkurugenzi wa Uchaguzi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi, Khalist Luanda alisema kurudufu karatasi za kupigia kura kunatakiwa kufanyika katika wilaya au mkoa lakini siyo nje ya mkoa.
“Ni kosa kuchapa fomu za wagombea kutoka wilaya moja kwenda nyingine walipaswa kurudufu katika eneo kunapofanyika uchaguzi au wilaya husika na mchakato unaopaswa kuwa wa siri sana na siyo kila sehemu kwani haitakuwa rahisi kusafirisha kwa usalama bila kutiliwa shaka.”
Aliongeza kuwa: “Nimesikia katika vyombo vya habari na nimetuma wataalamu wangu kwenda kufuatilia jambo hilo kwani ni makosa na mkurugenzi huyo inaonyesha alikuwa na malengo au masilahi binafsi na kama ni kweli anatakiwa kuwajibika.”
Awali akisimulia tukio hilo Mollel alisema: MwanaChadema alikwenda pale kurudufu karatasi zake kwani gharama yake ni Sh25 kwa karatasi moja na aliambiwa arudi jioni kwani walikuwa na kazi maalumu, hivyo wasingeweza kumrudufia karatasi zake.”
Aliongeza: “Alipokwenda tena saa 12 aliambiwa bado hawajamaliza kazi hiyo maalumu hapo alipata hofu na kuanza kuchunguza kazi iliyokuwa ikifanyika, ndipo alipoona karatasi za kupigia kura zikirudufiwa.”
Mollel alifafanua kuwa alipoona hivyo mfuasi huyo aliwaita wanachama wengine wa Chadema waliozingira duka hilo lililopo maeneo ya Mabibo kabla ya kutoa taarifa Kituo cha Polisi Mabibo umbali wa takriban mita 100.

Alisema polisi wa Mabibo na baadaye wa Magomeni walipofika waliwachukua wahusika na kuwapeleka Kituo cha Polisi Magomeni kwa ajili ya kuandika maelezo.
Shuhuda ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema: “Niliingia dukani hapo nikakuta wanachapisha hizo karatasi, lakini sikujali sana kwani nilikuwa nina haraka zangu, lakini baadaye niliporudi nikakuta baadhi ya hizo nyaraka zikiwa mezani na ndipo nikagundua kuwa ni nyaraka za siri ambazo hazitakiwi kuonekana kwa muda huo.”
Wakati huohuo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki alisema maandalizi kwa ajili ya uchaguzi huo yamekamilika kwa vifaa vyote kufika katika maeneo yatakayotumika kwa uchaguzi huo.
Alisema jumla ya wenyeviti wa mitaa 559 na wajumbe 2,795 wanatarajiwa kuchaguliwa. Jumla ya vituo 1,674 vya kupigia kura vitatumika huku masanduku yakiwa 5,022 na karatasi za kupigia kura zikiwa 1.7 milioni.
“Vituo vitafunguliwa kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 10 jioni, tunawaomba wananchi waliojiandikisha wajitokeze kupiga kura lakini wazingatie taratibu na sheria za uchaguzi,” alisema Sadiki.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema, “Kila chama kihakikishe hakivunji sheria kwani hatutakuwa na hiana na mtu yeyote, ukienda kinyume tutakuchukulia hatua kali bila kujali chama ulicho na wadhifa wako.”
Aliongeza: “Tunawaomba wanawake ambao mara nyingi wamekuwa waoga kwenda kupiga kura wakihofia usalama wao kujitokeza kwa wingi kwani tumejipanga vizuri kiulinzi kuhakikisha uchaguzi unaanza na kumalizika salama.”

ROSE MHANDO" MIMBA YA 4 BABA TOFAUTI"



Mapema wiki hii, chanzo kimoja kilipiga simu katika chumba chetu cha habari na kusimulia kuhusu habari hiyo, kwamba, Rose ambaye hana mume, amenasa na muda wowote kuanzia sasa anaweza kuitwa mama.
KUMBE
Madai ya chanzo hicho yalieleza kwamba, staa huyo amekuwa akijichimbia nyumbani kwake mkoani  Dodoma tofauti na siku za nyuma ambapo alikuwa hakauki jijini Dar.
“Kama hamsadiki ninayowaambia, najua ninyi mmebobea kwenye habari za uchunguzi ‘so’ fanyeni yenu mtaniambia,” kilidai chanzo hicho kikiomba chondechonde kisichorwe jina gazetini.

KUJIRIDHISHA
Ili kujiridhisha na habari hiyo, pasipo kwanza kuwasiliana na Rose, moja kwa moja, gazeti hili lilimpigia simu mmoja wa watu wa karibu wa nyota huyo (jina linahifadhiwa), alipopatikana, aliulizwa kuhusu ishu hiyo na haya ndiyo aliyoyaeleza:
Rose Muhando akipafomu na madansa wake.
“Yaani hadi leo mlikuwa hamjapata hii habari? Mimi siku zote nilikuwa najua labda kwenu siyo habari kwa sababu ujauzito huu ni wa siku nyingi. “Hata sasa hivi ukimuona alivyo unajua wazi kuwa kuna kichanga tumboni kwani tumbo limechomoza hatari.”
Mtu huyo wa karibu alisema anapokuwa nyumbani Dodoma mara nyingi amekuwa mtu wa kukaa ndani tu kutokana na watu kumshangaa.Alisema Rose amekuwa akijificha kwa sababu ya kuogopa macho ya watu na uchovu unaotokana na hali aliyonayo ‘kuchoka’.
NANI MHUSIKA?
Juu ya nani mhusika wa mimba hiyo, mtu huyo wa karibu, ambaye anafahamu kila kinachofanywa na nyota huyo wa Wimbo wa Facebook alisema kuwa, inadhaniwa kuwa ni ya mcheza shoo wake (jina kapuni).
Inadaiwa kwamba, Rose, mara kadhaa amekuwa akisisitiza kuwa ni lazima amzalie mtoto jamaa huyo kwa jinsi anavyompenda.“Huyo mcheza shoo ana uhusiano naye kwa muda mrefu kidogo na ameshasema kwa watu wengi tu kwamba endapo Mungu atapenda basi atafurahi kama atamzalia mtoto.
“Mimi hajaniambia mimba hasa ni ya nani, lakini naziona dalili zote kuwa ni ya huyo kijana,” alisema mtu huyo.
Rose Muhando na madansa wake wakitoa burudani.
MWENYEWE ANASEMAJE?
Baada ya kujiridhisha na maelezo ya mtu wake wa karibu, gazeti hili lilianza kumtafuta Rose, mama wa watoto watatu ambao wote amezaa na wanaume tofauti, lakini katika hali ya kushangaza, simu yake iliita hadi kukatika bila kupokelewa, hata baada ya kupigwa mara kadhaa.
Likiamini huenda alikuwa katika shughuli au mahali panapombana kuzungumza, gazeti hili lilimtumia ujumbe mfupi wa maneno (SMS) na kumsomea mashitaka hayo ili atoe ufafanuzi, lakini pia hakuweza kujibu.
Likiamini huenda simu yake haisomeki kwa mtumishi huyo wa Mungu, gazeti hili lilitumia simu nyingine ambayo nayo iliita kwa muda mrefu hadi kukatika pasipo kupokelewa na hata pia alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu wenye maelezo kuhusu hali yake ya sasa, pia haukujibiwa hivyo jitihada zinaendelea.
NI MTOTO WA NNE
Endapo itathibitika, ujauzito wa Rose utakuwa ni wa mtoto wa nne ambapo mara kadhaa staa huyo amekuwa akisema hayupo tayari kuolewa hivyo kuwaacha baadhi ya watumishi midomo wazi wakiamini mtu wa sampuli yake haifai kuzaa nje ya ndoa.

WANAODHANI MAISHA MAZURI YANATOKANA NA KUJIUZA BASI NAO WAJIUZE" HUDDAH MONROE"


Mshiriki wa zamani wa BBA Huddah alikasirika Baada ya mashabiki wake wa kike instagram kumwambia kuwa anatembea na wanaume wengi ili ili apate pesa ya kuishi.

Naye akaamua kuwajibu kuwa kama wanafikiri maisha mazuri aliyonayo yanatokana na yeye kujiuza basi na wao wajiueze ili wawe na maisha kama yake.

Hii yapa Comment yake

"Honestly, I don't understand why women have to be the ones hating all the damn time . If you think my v@gina is giving me the life I live then why don't u use your vagina too to get a life instead of hating?"

DIAMOND PLATINUMZ HATAREE, APOKELEWA KAMA MFALME DAR AKITOKEA SOUTH.



Diamond baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar.
Mashabiki waliofika uwanja wa ndege kumpokea Diamond.
Diamond akipokelewa na mashabiki kwa shangwe.
MWANAMUZIKI Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' ametua nchini muda huu akitokea Afrika Kusini alipokwenda kushiriki zoezi la utoaji tuzo za Channel O ambapo alijinyakulia tuzo tatu kwa mpigo. Tuzo alizonyakua staa huyo ni pamoja na Most Gifted New Comer, Most Gifted Afropop na Most Gifted East kupitia wimbo wake wa Number One.

AL SHABAB WAMFANYA IGP KIMAIYO WA KENYA AJIUZULU


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kenya, David Kimaiyo ametangaza kustaafu leo kutokana na shinikizo dhidi yake ajiuzulu kwa kushindwa kukabiliana na usalama nchini humo.
Wakati huohuo Kenyatta amempendekeza Waziri Mkuu mpya wa usalama Joseph Nkaiseri kuchukua nafasi ya aliyekuwa Waziri wa Usalama wa nchi hiyo, Joseph Ole Lenku.
Rais Kenyatta alisema kuwa baada ya mazungumzo na Bwana Kimaiyo alikubali kustaafu majukumu yake hayo.

KWA HILI MPENZ WA WOLPER ARINGE TU...


Ni jambo la kawaida kwa binadam kujiachia hasa pale tunapokuwa katika hali fulan ya raha ama kujawa na hisia nzuri za kimahaba. Kupitia akaunti yake ya Instagram, msanii wa Bongo Movie, Mrembo Jacqueline Wolper amefunguka na kusema kuwa hlo ndio pozi analohusudu pindi anapokuwa ana chat na wake wa moyo.....

Je wewe ushawahi kujitathmin kuhusiana na pozi gani hukuhamasisha unapokuwa unawasiliana na mwenza wako...???

JANGA LA UPUNGUFU WA NGUVU NA MATUMIZ YA VIAGRA KWA WANAUME


Inasikitisha sana siku hizi wanaotumia Viagra ni vijana wadogo sana ,wengine hata ni wanafunzi wa vyuo. Na hii si Dar tu, mpaka hata mikoani..nilikua Dodoma nikawa na jamaa yangu mmoja pale anaduka la dawa...ananiambia Viagra ndio inamlipa kuliko dawa zote.

Wateja ni wanafunzi wa vyuo na waheshimiwa. Sijui kwa kweli nini kinalikumba Taifa. Hivi kweli kwa mawazo yako unaweza ikomoa papuchi wewe. Acheni ujinga jamani.
Excellence is not a destination you arrive at… It is the benchmark for your journey. Earvin “Magic” Johnson

SAKATA LA ESCROW, KUMBE LUKUVI ALITAKA KUIBA RIPOTI SAA 9 USIKU.


Dar es Salaam. Viongozi wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe na Deo Filikunjombe wamemtuhumu Waziri William Lukuvi kuwa alitaka kuiba ripoti ya kamati yao kuhusu uchotwaji wa Sh306 bilioni kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow.
Sakata hilo lilihitimishwa Jumamosi wakati Bunge lilipoazimia kuwajibishwa kwa watu wote waliohusika kwenye uchotwaji wa fedha hizo, ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa taasisi za fedha zilizoruhusu kufanyika kwa miamala mikubwa kinyume na taratibu za kibenki. Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, wabunge hao wawili kutoka Chadema na CCM walilieleza gazeti hili kuwa jaribio hilo lilishindikana baada ya wao na mjumbe mwalikwa, Luhanga Mpina (CCM) kuamua kukesha wakiilinda ripoti hiyo tangu ilipokuwa ikichapwa hadi ilipowasilishwa bungeni.
Hata hivyo, Lukuvi alikanusha vikali tuhuma hizo akisema kuwa aliipata ripoti hiyo siku iliposomwa na kwamba kama angehusika, asingekubaliwa kuwa mjumbe wa kamati ya maridhiano iliyoundwa mwishoni mwa kikao kupendekeza maazimio ya Bunge.
“Si kweli,” alisema waziri huyo wa nchi anayehusika na sera, utaratibu na Bunge.
“Unajua PAC walikuwa wanafanya kazi chini ya hazina. Hata Spika wa Bunge hakuiona hiyo ripoti, aliisikia tu ikisomwa bungeni. Kwanza kamati ilikuwa ikidurufu hiyo taarifa yake eneo la mbali na ili uipate ilikuwa ni lazima umrubuni Zitto.”
Aliongeza kusema: “Kama kweli nilikuwa nataka kuiba taarifa yao nisingekubali kuwa mmoja wa wajumbe wa kamati ya maridhiano, iliyokutana kupitia upya mapendekezo ya PAC baada ya yale ya awali kuzua mvutano bungeni.”
Hata hivyo, Filikunjombe, ambaye alikuwa makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, alikwenda mbali zaidi na kudai kuwa walilazimika kumwondoa eneo la kuchapishia ripoti hiyo. “Waziri Lukuvi alitumwa saa 9:00 usiku kuiba taarifa yetu wakati tunaichapa. Taarifa ilikuwa katika ‘flash’ na tulipogundua hilo tulimfukuza. Sisi tuliamua kuilinda ripoti ili isiibwe,” alisema Filikunjombe ambaye ni mbunge wa Ludewa kwa tiketi ya CCM.
“Ile taarifa tuliichapa usiku wa kuamkia Jumatano ambayo ilikuwa siku ya kuiwasilisha bungeni. Na hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya kikao cha Bunge kuahirishwa mara tu baada ya PAC kuwasilisha taarifa yake, ili Serikali ikajipange,” aliongeza.
Mbali na kauli yake ya jana, Filikunjombe aligusia suala hilo la ulinzi wakati akishukuru wabunge kwa kushikamana katika kufikia maazimio manane ya kuwawajibisha wote waliohusika.
Katika shukrani hizo, Filikunjombe alisema walilazimika kukesha usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita kuilinda ripoti yao isiibiwe na hivyo kuwashukuru watendaji wa Bunge kwa kazi nzuri.
Hata hivyo, kabla ya kuwasilishwa kwa ripoti hiyo kulienea taarifa kuna watu waliiiba na kunyofoa kurasa zilizokuwa na nyaraka za vielelezo na baadaye kuanza kuzisambaza. Polisi ilidai baadaye kuwa ilimkamata mtu aliyekuwa akisambaza vitabu hivyo vya ripoti, lakini hadi leo hajafikishwa mahakamani wala hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na polisi kuhusu maendeleo ya mtuhumiwa huyo.
Katika sakata hilo kubwa la aina yake, Bunge limtia hatiani Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Mwanasheria Mkuu Jaji Fredrick Werema na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Eliachim Maswi na wakurugenzi wa Shirika la Umeme kwa kuhusika kwa makusudi au kwa uzembe katika kufanikisha miamala haramu kutoka kwenye akaunti hiyo.

AKODI MATARUMBETA KWENDA KUMSUTA MWIZI WA BWANA WAKE WA ESCROW


Makubwa! Wakati Wizara ya Nishati na Madini ikiwa kwenye msukosuko wa fedha zilizochotwa ‘kihuni’ kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, mwanaume mmoja, mtumishi wa wizara hiyo mkoani hapa almaarufu Kigogo wa Escrow, amesababisha wanawake wawili kusutana kwa matarumbeta na kukabana wakidaiwa kumgombea kwani ana fedha ‘chafu’.
Wakina mama, Tabu Mohamed na Mwajuma Chota  ( katikati ) wakisutana kwa kuibiana mabwana.
Tukio hilo la aina yake lilijiri wikiendi iliyopita katika Mtaa wa Karume mjini hapa ambapo wanawake hao, Tabu Mohamed na Mwajuma Chota walisababisha pakachimbika hadi polisi walipofika na kuokoa jahazi.
Awali ilifahamika kwamba wanawake hao walikuwa wakiishi pamoja maeneo ya Kikundi, Kata ya Sultan Area mkoani hapa. Kwa mujibu wa madai ya mashuhuda waliokuwa wamefunga mtaa huo, Tabu ndiye aliyeanza ‘kuchepuka’ na kigogo huyo ambaye ni mume wa mtu aliyemnunulia gari aina ya Toyota Opa.
Madai yaliendelea kushushwa kwamba, Mwajuma ambaye ni mke wa mtu alipoona mwenzake anakula vinono, naye akajiweka.
Bendi ilikodiwa na Tabu Mohamed ili kumsuta shosti yake Mwajuma Chota.
Habari za mtaani zilidai kuwa katika kujiweka, alifanikiwa kulamba mshiko wa shilingi elfu 80 kabla ya kushtukiwa na Tabu huku naye akitaka kuhongwa gari kama mwenzake.
Ilielezwa kwamba katika kufuatilia, Tabu aligundua kuwa Mwajuma anachepuka na ‘mshefa’ wake ndipo akapanga mashambulizi ya vita vya ardhini.
Kwa hasira, Tabu alishonesha sare za ‘madila’ na kununua mizinga ya pombe kali ambapo alienda kukodi matarumbeta na watu wa kusuta.
Wakubwa kwa watoto wakishuhudia vimbwanga vya wakinamama hao.
Ilisemekana kwamba kabla ya tukio, watu walipiga pombe kisha wakamfuata nyumbani kwao, Mtaa wa Karume na kulianzisha.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda ambalo liliwasili eneo la tukio ndani ya dakika sifuri juu ya tukio hilo, Mwajuma alifunguka: “Namshangaa Tabu kuja kunifanyia vurugu wakati na yeye ni mwizi tu. Huyo bwana ni mume wa mtu.”
Kwa upande wake, Tabu alidai Mwajuma ni shosti yake lakini alimtendea kitendo kibaya cha kutembea na bwana’ke.
Mmoja wa wamama hao, Tabu Mohamed  akichukuliwa na polisi kwa kumletea fujo mwenzake, Mwajuma Chota.
Alipobanwa zaidi hasa suala la kukodisha matarumbeta na kwamba mwanaume huyo ni mume wa mtu, Tabu alidai kwamba jamaa huyo alimkataza kuzungumza na wanahabari.
Baada ya kuipata ishu hiyo, gazeti hili liliwasiliana na mke wa kigogo huyo na kumuuliza kama ana habari kwamba kuna wanawake wanamgombea mumewe ndipo akapatwa na mshtuko na kuahidi kulifanyia kazi na kama ni kweli atafungasha virago.
Makamanda wa Polisi wakiimarisha ulinzi eneo la tukio.
Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Karume, Elly Mgota alithibitisha vurugu hizo kutokea kwenye mtaa wake ambapo sakata hilo lilitinga polisi baada ya Tabu kutiwa mbaroni kwa kosa la kumfanyia fujo mwenzake.

KESI YA MADAWA ILIVYOHARIBU MIPANGO MIZURI YA CHID BENZ


Rapper Chidi Benz anayekabiliwa na kesi ya kukutwa na madawa ya kulevya, amesema kesi hiyo imeathiri kufanyika kwa video ya wimbo wake ‘Mpaka Kuchee’ aliyowashirikisha Diamond na AY.

Chidi alikuwa akiongea na Bongo5 jana kwenye uzinduzi wa video ya Wakazi ‘Wanawake wa Dar’.

“Video inakuja, bado sijaanza kufanya mazungumzo na AY wala Diamond ambao nipo nao kwenye hiyo project,” alisema. Video itafanyika hivi soon, haya matatizo ndo yameichewesha hii project.”

Kesi yake inatarajiwa kusikilizwa tena December 1. Diamond na AY waliahidi kugharamia video hiyo.

Credit Bongo5

AJALI ILIYOTOA UHAI WA MMILIKI WA MATEI LODGE NA KUMJERUHI BLOGGER WA DODOMA


Gari alilokuwemo Mattei likiwa limeharibika vibaya baada ya ajali.
Wananchi wakiwa eneo la tukio.…
Gari alilokuwemo Mattei likiwa limeharibika vibaya baada ya ajali.
Wananchi wakiwa eneo la tukio.
Mmiliki wa Mattei Lodge enzi za uhai wake.
MMILIKI wa Mattei Lodge iliyopo Area D mkoani Dodoma aliyefahamika kwa jina moja tu la Mattei amefariki dunia katika ajali ya gari jana Jumapili eneo la Pandembili, Kongwa.
Chanzo cha ajali hiyo inadaiwa kuwa mwendo kasi uliopelekea gari hilo kuligonga gari lingine na kisha kupinduka.
Marehemu Mattei alikuwa na wenzake watatu katika gari ambao walijeruhiwa Akiwemo Blogger wa Dodoma Boss Ngassa.

ASKARI WA JWTZ APIGA MTUNGI MPAKA KUJIKOJELEA NA KUTUPWA MTARONI


KATIKA hali isiyotegemewa askari mmoja wa jeshi la kujenga Taifa (JKT) anayesadikika kuwa na wa kambi ya Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa usiku wa leo amenusurika kuvuliwa nguo za jeshi hadharani baada ya kukutwa amelewa chakali na kulala katika mfereji wa maji machafu eneo la nje ya stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani mjini Iringa
Tukio hilo lilitokea muda wa saa 2 usiku baada ya wasamaria wema kumshusha askari huyo kutoka katika basi la Mgumba ambalo alikuwa amepanda kutoka Mafinga kuja mjini Iringa.
Akisimulia kisa na mkasa wa askari huyo kulewa chakali kiasi cha kushindwa kujitambua mmoja kati ya wasamaria wema aliyejitolea kumshusha katika basi hilo alisema kuwa askari huyo alipanda basi hilo Mafinga huku akiwa amelewa na wakati wote wa safari alionekana akinywa pombe kali kiasi cha kushindwa kujimudu na kuanza kutapika na kujisaidia haja ndogondani ya basi hilo.
Hata hivyo alisema baada ya kufika stendi ilikuwa ni vigumu kujitambua hivyo kupoteza fahamu na kulazimika kumpa msaada na kumzimua kwa maji kabla ya kupata fahamu kiasi na kujificha chini ya mfereji wa maji machafu .
Alisema kuwa mara baada ya kujitambua kiasi aliweza kutoa namba ya ndugu yake ambae ni askari wa FFU mjini Iringa aliyefika kumnusuru kuvuliwa nguo na kiongozi wake aliyefika eneo hilo na kumkutana akilishushia heshima jeshi kwa ulevi uliopitiliza
" Umelidhalilisha sana jeshi kwa askari kulewa hivi ukiwa katika sare .....sasa nataka kukuvua sare kisha nakupeleka kulala polisi kabla ya kesho kukuchukulia hatua zaidi " alisikika akisema kiongozi huyo ambae jina wala cheo chake hakukitaja
Maamuzi hayo ya kiongozi wake yaliwafanya mashuhuda kumuangukia na kumwomba amsamehe kwani bado ni kijana mdogo sana mambi ambayo aliyakubali na ndugu zake kumpakiza katika Taxi na kumpeleka eneo la Kihesa .
Ushauri wetu kwa askari wetu kujaribu kuheshimu nafasi hizo japo hakuna anayewakataza kunywa pombe ila watambue kuwa unywaji pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako ama chonde chonde ulevi noma.


HISTORIA YA SINGA SINGA TAPELI WA IPTL AMBAYE ANALIWEKA PABAYA TAIFA



Unamjua? Anaitwa Harbinder Singh Sethi! Ni mfanyabiashara bilionea mwenye asili ya Bara la Asia na mmiliki wa mtambo wa kufua umeme wa Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ambayo hivi karibuni imezua tafrani Bongo kufuatia kampuni yake kuhusishwa na uchotwaji wa fedha kiasi cha Sh. Bilioni 306 kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Singa singa ambaye ni mmiliki wa mtambo wa kufua umeme wa IPTL, Harbinder Singh Sethi! (wa pili kulia) akielekeza jambo.
Harbinder ambaye ni singasinga anatajwa pia akidaiwa kuwa mfanyabiashara tapeli kufuatia vitendo vyake mbalimbali katika kumiliki makampuni na ukwepaji wa kodi ya serikali.
HISTORIA YAKE FUPI
Harbinder anatajwa na vyanzo kwamba ni mzaliwa wa Mkoa wa Iringa. Mwaka 1977 akiwa na umri wa miaka 20 ya kuzaliwa na nduguze wawili, Nota Singh na Manjit Singh walianzisha kampuni ya ujenzi wa barabara iliyojulikana kwa jina la Ruaha Concrete Co. Ltd ikitumia SLP 498, Iringa. Ruaha ni sehemu maarufu kwenye Manispaa ya Mji wa Iringa kukiwa na vitongoji vya Ipogoro, Kibwabwa na Ndiuka. Jina la Ruaha linatokana na Mto Ruaha kupita eneo hilo.
Vyanzo vinasema, Harbinder alianza kumiliki fedha nyingi kuanzia miaka ya 80 wakati familia ya Rais wa Kenya wakati huo, Daniel Arap Moi ilipoanza kujiingiza kwenye biashara mbalimbali.
Waziri mkuu, Mh. Mizengo Pinda.
AHAMIA KENYA
Vyanzo vikadai kuwa, miaka hiyo, singasinga huyo alihamia jijini Nairobi, Kenya ambako alianza kuwa mshirika wa kibiashara na mtoto wa kwanza wa Rais Moi aitwaye Gideon Moi.
ALIANZA UMEME NCHINI KENYA
Akiwa nchini humo, vyanzo vinamtaja singasinga huyo kuwa alipata umiliki wa mtambo wa Westmont wa kuzalisha umeme wa megawati 47 jijini Mombasa.
Washirika wenzake katika mradi huo walikuwa Mukesh Gohil, Kamlesh Pattni, Gichuru na Mkurugenzi Mtendaji wa KPLC, Mutitu.
Singh pia anatajwa kuwa na miradi  74 iliyofungwa katika maeneo mbalimbali ya Afrika Mashariki kutokana na kuvurunda kama siyo kufanya vibaya.
ALIPATA MSALA KENYA
Mwaka 1997, Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Mashirika Kenya ilianika udhaifu wa Ruaha Concrete katika tenda ya ujenzi wa barabara ambako kulikuwa na ucheleweshaji, kuongezeka kwa gharama pamoja na utekelezaji hafifu uliojitokeza.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi.
Kufuatia madai hayo, ilibidi mhandisi msimamizi wa mradi huo aliyetajwa kwa jina moja la Kitololo ajiuzulu baada ya kukataa kutia saini kuwa kazi iliyozembewa imekamilika.
ARUDI BONGO
Haikujulikana mara moja ni mwaka gani alirejea Bongo, lakini ilidaiwa kuwa tayari alishawekeza nchini huku akiwa bado ana biashara zake Kenya na baadaye alirudi jumla kutokana na misala ya kule.
KWA NINI NI TAPELI?
Singh anatajwa kuwa mfanyabishara tapeli kufuatia Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kumtaja kuwa amehusika na vitendo vya ukwepaji wa kodi akitumia mbinu za ujanjaujanja.
Mfano mkubwa ni hizo bilioni 306 alizochota kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow hakuzilipia kodi na ndiyo maana Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akihutubia bunge mjini Dodoma, Ijumaa iliyopita katika mjadala huo aliamuru kodi hiyo ilipwe mara moja.
Lakini pia kwa mujibu wa TRA na Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), jamaa huyo amekuwa na tabia ya kuuza hisa kwa bei ya chini kwa makampuni mengine ili aweze kulipa kodi ndogo jambo ambalo pia ni kuonesha ni mfanyabiashara tapeli.
Jaji Werema akiteta jambo na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila.
Kamati ya Zitto Kabwe ambaye ni mwenyekiti wa PAC, pia ilibaini kuwa, wakati yeye alijulikana kuwa ndiye mmiliki wa Kampuni ya IPTL ambayo baadaye aliiuza kwa Pan African Power Solutions Limited (PAP), uchunguzi wa PAC ukaja kubaini kuwa, mwenye PAP ndiyo huyohuyo mwenye IPTL, yaani singasinga huyo. Dah!
ALIHENYESHA BUNGE LA TANZANIA
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Bongo, Ijumaa iliyopita bunge liliendeshwa hadi saa 5:00 kasoro usiku, ishu ikiwa ni kujadili yaliyotokana na Kamati ya PAC baada ya kuchunguza wizi wa mabilioni ya shilingi kutoka Escrow kwenda IPTL kwa kupitia PAP.
Baadhi ya mawaziri na vigogo serikalini ambao wengine walimwaga machozi kutokana na kashfa waliyoipata kupitia Kampuni ya IPTL hawatamsahau singasinga huyo kwa vile amewaingiza kwenye kumbukumbu mbaya ya Taifa la Tanzania. Katika listi ya viongozi hao yumo Mizengo Pinda, Profesa Sopspeter Muhongo, Stephen Masele, Eliakim Maswi, Jaji Feredrick Werema na wengine wengi.
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, Spika wa Bunge, Anne Makinda aliliahirisha bunge hadi Januari, mwakani katika kikao cha 18 bila kumwadhibu mtu juu ya sakata hilo.
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga