Waislamu nchini Norway wakiweka mviringo wa kuwazunguka wayahudi ili kuonyesha amani kufuatia misururu ya mashambulizi inaowalenga raia hao.
Zaidi ya watu 1000 wengi wao wakiwa  waislamu wameunda mviringo na kulizunguka sinagogi nchini Norway  kuonyesha umoja wao kufuatia mashambulizi kadha yaliyowalenga wayahudi  barani Ulaya.
Wakati waumini wa kiyahudi walipokuwa  wakitoka ndani ya sinagogi katika mji mkuu wa Norway Oslo kulikuwa na  shangwe wakati vijana wa kiislamu walipowazingira kama ishara ya amani.
Warsha hiyo ilipangwa na vijana wa kiislamu na inafanyika wiki chache baada ya kijana mmoja mzaliwa wa Denmark mwenye asili ya Kipalestina kuwaua watu wawili.
Warsha hiyo ilipangwa na vijana wa kiislamu na inafanyika wiki chache baada ya kijana mmoja mzaliwa wa Denmark mwenye asili ya Kipalestina kuwaua watu wawili.
(Chanzo: BBC)