SHIRIKA la Afya Duniani (WHO), limetoa takwimu mpya za ugonjwa wa Ebola ambapo mpaka sasa watu 8,795 wamefariki huku 22,057 duniani kote wakiwa wameambukizwa virusi vya ugonjwa huo.
Katika takwimu hizo, nchi ya Sierra Leone ina jumla ya watu 10,518 wenye virusi vya Ebola, Liberia watu 8,622 na Guinea 2,917.
Nchi nyingine ambazo maambukizi yake yapo chini ni Nigeria yenye maambukizi ya watu 20 huku vifo vya watu nane vikiripotiwa, Mali maambukizi ya watu nane huku waliokufa wakiwa sita. Marekani yenye maambukizi ya watu wanne huku mmoja akifariki.
Senegal, Hispania na Uingereza kila moja ina mtu mmoja…

Senegal, Hispania na Uingereza kila moja ina mtu mmoja aliyeambukizwa huku zikiwa hazina vifo.
Liberia ndiyo nchi inayoongoza kwa vifo ambapo watu 3,686 wamefariki, huku Sierra Leone ikiwa na vifo 3,199 wakati Guinea ikiripotiwa kuwa na vifo 1,910.
Maambukizi ya ugonjwa wa Ebola yamepungua kwa sasa tangu yalipoanza mwezi Machi 2014 huku baadhi ya wataalamu wakieleza kuwa ugonjwa huo unaweza kuwa umetokomezwa kabisa ifikapo Mwezi Juni mwaka huu.