Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

BREAKING NEWS :MEZ B AFARIKI DUNIA


Msanii Mez B aka Moses aliyekuwa Mkoani Dodoma kwa matibabu baada ya kurudishwa nyumbani na mama yake amefariki Dunia. Mez B alikuwa akiuguliwa na homa ya mapafu [Pneumonia] na alikuwa kwenye dozi na leo ilikuwa siku ya tatu toka anatumia dawa hizo. 



Leo asubuhi aliamka na kunywa dawa na chakula ila hali yake haikuwa sawa na kuonekana amelegea. Daktari wake alipigiwa siku na kuamuru awekewe drip ila hali yake ikawa mbaya zaidi, wakati wanampeleka hospitalini alifia walipofika mapokezi. Jirana amelezea haya. 

Pole kwa familia ya Mez B, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema, Amen

BAADA YA KUONEKANA PICHA ZA UTUP# ZA NAY AKIWA NA KIMWANA, WADAU WAMPA UJUMBE HUU.


 
KWAKO mkali wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’. Mambo vipi? Mishe zinasemaje? Binafsi mimi ni mzima wa afya, maisha yanasonga mbele kwa kasi ya ajabu. Tunapambana!Nimekukumbuka leo kwa barua maana kitambo kidogo hatujaonana. Nakupongeza kwa nyimbo zako maana hata wale waliosema ulibebwa na Diamond katika wimbo wa Muziki Gani, sasa hivi wanajutia kauli zao.
Wanaona walikosea maana umefyatua nyimbo zako mwenyewe na unaendelea kukimbiza mitaani.
Madhumuni ya barua hii ni kutaka kukueleza kwamba wewe ni staa hivyo unapaswa kuwa mfano wa kuigwa na kila mtu katika jamii. Hutakiwi kuteleza hata kidogo. Ukiwa wewe ndiyo kinara wa majanga, utatolewa mfano kwamba hufai kuigwa kutokana na matendo yako maovu.

Kila mmoja anatambua uwezo wako, anatambua hatua ambayo umefikia kimuziki. Watu wanatambua kwamba una mchumba ambaye una mikakati ya kufika naye mbali kwa maana ya ndoa Mungu akipenda.
Kinachoshangaza ni kwamba, inakuwaje unaonekana katika pozi za kimahaba na mwanamke mwingine? Picha zenyewe zinatia kinyaa?
Mwishoni mwa wiki iliyopita gumzo katika mitandao ya kijamii ilikuwa ni wewe na picha zako za utup# na mwanamke huyo ambaye hakuwa mchumba wako.Ndugu yangu, picha zile hazikuwa nzuri kwako. Zimekudhalilisha na hata kukuletea ugomvi kwa mchumba wako.
Kwa nini ulikubali kupiga picha za namna ile? Zilikuwa za nini? Ulikuwa na malengo gani? Hata kama mlikuwa katika ‘shooting’ ya wimbo kwa nini ulikubali kupigwa picha katika hatua ile?
Tena bora zingevujishwa na mtu mwingine, wewe mwenyewe unatajwa kuwa ndiye chanzo cha kusambaa kwa picha hizo kupitia mitandao yako ya kijamii, hivi kwenye kichwa chako uliwaza kabla ya kufanya?
Unapaswa kujiheshimu hata kama ni video ya wimbo, naamini kwa desturi zetu, kamwe huwezi kuruhusiwa kurusha video ya namna hiyo hewani. Tamaduni zetu haziruhusu, unasubiri nani akuzuie kufanya hivyo wakati wewe kama kioo cha jamii unapaswa kuwa mfano?
Una watoto sasa, ulimwengu wa sasa si ule wa zamani. Picha zako za utupu zinachapishwa magazetini, zitasambaa kwenye mitandao mbalimbali na wanao pia watajionea bila wasiwasi. Watajifunza nini kutoka kwa baba? Jibu najua unalo na haliwezi kuwa zuri kwa mtu muungwana.
Ulimwengu wa sasa, ukifanya vituko vya namna hiyo, rekodi zake zinabaki kwenye mitandao. Vizazi na vizazi vitakuja kuona hayo uliyoyafanya juzi. Badilika kaka!Ni matumaini yangu utakuwa umenielewa, kwa leo naishia hapa, naamini utafanyia kazi mawazo yangu na kubadilika.
Wasalaam,

WABONGO WANAWAPA ULAJI SANA WA SOUTH" AY


Yessaya ‘AY' akipozi.
Stori: Shani Ramadhani
STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Ambwene
Yessaya ‘AY’ amefunguka kuwa maprodyuza
wengi waliopo Afrika Kusini ‘Sauz’
wanapata faida kubwa sana kutoka nchi za
Afrika hasa Tanzania kupitia muziki.
Akichonga na Over The Weekend, AY alisema
wasanii walio wengi kutoka Bongo
wamekubaliana
na gharama zao ndiyo maana wanakwenda
kurekodi huko kuanzia ‘audio’ mpaka video.
“Sauz sasa hivi imekuwa kama moyo wa
muziki kwa Wabongo kutokana na kila
mmoja kukimbilia huko kwa sababu tu kuna
waandaaji wengi wa muziki.
Wanawanufaisha sana, natamani na sisi
siku moja Wasauz wakimbilie Bongo
kurekodi,” alisema hj

RAY C KUMSAIDIA DAZ BABA KUPONA "UTEJA"


Staa wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ameapa kumsaidia mwanamuziki mwenzake David Jacob ‘Daz Baba’ anayedaiwa kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya. 

Chanzo cha kuaminika kimeeleza kuwa, Ray C amekuwa akiumizwa na hali aliyonayo Daz Baba na amefanya kila awezavyo hadi kuongea naye ili aanze kutumia dozi ya Methadone ambayo wengi huipata katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar.

“Ni kweli hali ya Daz Baba inasikitisha na Ray C huyuhuyu unayemjua kaongea naye na amemshawishi kuanza kutumia dozi,” kilidai chanzo hicho ambacho ni rafiki wa Ray C.
Baada ya kuzipata taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta Ray C, alipopatikana alikiri kuanza mazungumzo na Daz ila akaomba asizungumzie walipofikia kwa sasa.


KWELI BODY GUARD WA DIAMOND NI NOUMAH, ANGALIA MBWEMBWE ZAKE HAPA.


Kwa tetesi tunazosikia huyu jamaa ndo mlinzi binafsi wa wasanii wa hapa Tanzania anayelipwa ghali zaidi. kuanzia mshahara na marurupu mengine kiasi kwamba anaishi kama majuu vile. Si haba kama shukrani yake kuendelea kukitunza kibarua chake kwa kuji keep well fit kila mara.

Angalia baadhi ya picha zake hapo chini ikiwa kikazi zaidi:-




ALI KIBA AKIRI KUWA NA BEEF NA DIAMOND PLATINUMZ, AFUNGUKA.


Hatimaye staa wa Bongofleva Ali Kiba amekiri kuwa yuko katika bifu na mwanamuziki mwenzie Diamond Platnumz kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.
Kauli hiyo ya Ali Kiba inapingana na ile ya hivi karibuni iliyowahi kutolewa na Mwenyekiti wa Kamati za bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe alisisitiza kuwa wanamuziki hao hawana tofauti zozote na kwamba ni watu tu ndio wanakuza suala hilo.
Hata hivyo, juzi Ali Kiba aliliambia gazeti hili kuwa ni kweli kuna ugomvi baina yao, huku akisisitiza kwamba tofauti yao ilianza mwaka 2012. Wakati Ali Kiba akifunguka kuhusu bifu hilo hali imekuwa tofauti kwa Diamond ambapo amekaririwa mara kadhaa kuwa hana tofauti yeyote na mwanamuzi huyo ambaye wanatoka mkoa mmoja wa Kigoma na kuunganisha Kundi la Kigoma All Stars. Akizungumza wakati akijibu maswali mbalimbali katika mahojiano maalumu, mwanamuziki huyo pia alielezea mambo mengi kuhusu muziki wake na hii ni sehemu ya mahojiano hayo;
Swali: Nini chanzo cha bifu lako na Diamond?
Ali Kiba: Hakuna kiini kwa sababu nadhani hayo mimi aaah.…Kiukweli haya tuliyamalizaga muda mrefu …Labda watu wahisi kwamba kipindi kile alichonifuta katika wimbo wake (alisema bila kufafanua jina la wimbo) na yeye alivyosema kwamba nimemfuta katika wimbo wangu ‘Single Boy’, mimi sijawahi kurekodi na Diamond katika wimbo wangu hata mmoja na huo niliimba na Lady Jaydee.
Yeye ndiye aliyesema kwamba nilimfuta katika wimbo ule, ila ukweli ni kwamba hatukuwahi kuingia pamoja studio, nilimshauri tufanye wimbo mwingine lakini siyo ule kwa sababu nimeshaimba na Lady Jay Dee.
Swali: Umeshawahi kuwa karibu na Diamond?
Ali Kiba: Hapana yeye ndiyo alishawahi kuwa na ukaribu na mimi.
Swali: Unaweza kufanya kolabo na Diamond?
Ali Kiba: Ngoja nikwambie ukweli, sidhani kama ninaweza kuja kufanya kolabo na Diamond, ila nikipata wimbo ambao nadhani kwamba anastahili kuwapo, kiukweli nitamshirikisha lakini kama hastahili haitawezekana.
Kwa sababu kila wimbo unajielezea, kwa mfano kama mtu anataka kufanya Zouk akimtafuta Stara Thomas itawezekana kwani hayo ndiyo mambo yake, kwa hiyo kama nikitaka kufanya naye wimbo ambao nitaona kwamba unafaa nitamfuata na nitamweleza.


Swali: Utofauti kati yako na Diamond ni upi?
Ali Kiba: Mimi naimba muziki mzuri na nina ‘hit song’, naye Diamond anaimba ‘hit song’, unaposema mimi sina hit song wakati mimi nina nyimbo nyingi kushinda yeye unakuwa unakosea, tangu nimeanza kuimba ni nyimbo mbili tu hazijawahi kuwa hit ikiwamo ‘My Everything’ na ‘Mali Yangu’ lakini nyingine zote zilivuma tangu nianze kufanya muziki.
Swali: Inasemekana katika Tamasha la TigoMusic kuna hirizi zilionekana Uwanja wa Leaders na wewe na Diamond mnatuhumiwa kuhusika, unalizungumziaje?
Ali Kiba: Yaani Mungu mmoja sina imani hiyo kabisa na mimi naamini Mungu na mambo ya hirizi na mimi ni tofauti. Nadhani watu wanasema hivyo kwa sababu wanadhani kwamba kuna bifu. Binafsi sina bifu na msanii yeyote labda kama wanaweza kuwa na bifu na mimi binafsi simchukii msanii yeyote na sina bifu na yeyote.
Swali: Video yako ya Mwana imezungumziwa na mashabiki kuwa haikuwa na uhalisia. Pia ilikuwa ya kawaida sana, wewe binafsi unalichukuliaje?
Ali Kiba: Video ilivyokuwa ndivyo ilipangwa iwe kwa sababu kila mtu alikuwa amejenga picha itakuwaje kwa hiyo ililazimika kufanya vile kwa kuwa watu walishapanga mpaka gharama kwa kuwa nilikaa muda mrefu pasipo kufanya. Ningefanya kitu ambacho watu walikifikiria kiukweli ingekuwa karaha, nilichozingatia mimi ni kuimba vizuri na kuonyesha fikra za wimbo husika.
Swali: Vipi uliandaa ‘skripti’ ya video au aliamua GodFather kuifanya vile ilivyotengenezwa?
Kiba: Tulikuwa na ‘script’ yetu pia waongozaji wa video walikuwa na yao ambayo walitupatia. Hivyo tukakubaliana nao kwa sababu tulitaka kuleta utofauti na kila kitu kikakaa sawa.
Swali: Ni kweli kwamba una mpango wa kufanya kolabo na Chris Brown?
Ali Kiba: Uwezekano wa kufanya upo kwa sababu kila kitu ni mipango kwa hiyo naweza kufanya kolabo na wasanii wa kimataifa na mashabiki watarajie kufanya hivyo.
Swali: Kwa nini haujafanya video ya Kimasomaso na ulisema video ya Mwana ingefanyika Dar es Salaam kwa nini ulitengenezea Afrika Kusini?
Ali Kiba: Video ya ‘Kimasomaso’ ilishindikana kutokana na muda ulikuwa hautoshi, nilijikuta niko katika mambo mengi sana kwani nilikuwa nimeegemea katika video ya Mwana kwa hiyo nilipokuja kugeuka ikawa ni vigumu.
Nilisema kwamba nyingine ningefanya nje ya hapa lakini kwa ‘Mwana’ sijaelewa kwanini nifanye hapa, tofauti na hiyo nyimbo haikuwa na maana ya Dar es Salaam, maana yake ni mwanamke na mwanamume sikuona sababu ya kufanyia hapa jijini.
Ukitumia neno la Dar es Salaam ni kwa sababu ni jiji lenye changamoto kwa hiyo unapozungumzia hilo ina maana kwamba ni Joharnesburg, Nairobi, Kampala, London majiji ambayo yana changamoto mfano video ya Macmuga nilifanyia Marekani.
Source, Mwananchi.

FAMILIA YA RAPPER STEREO YATEKETEA KWA AJALI YA MOTO


Mama mdogo, Baba Mdogo,kaka yake Mjomba na watoto wa Kaka yake Rapper Stereo wamepoteza Maisha kwenye ajali ya moto iliyotokea leo maeneo ya Ukonga Banana jijini Dar Es Salaam
Hii ndiyo nyumba iliyoteketea kwam moto na kusababisha vifo vya mama mdogo,baba mdogo,kaka,mjomba na watoto wa kaka wa kaka yake rapper Stereo

Taarifa hii ilithibitishwa na watu wake wa karibu akiwemo Nikki Mbishi na Songa
"Nimefiwa nababa mdogo(last born wa marehemu baba yangu)mama mdogo,kaka,uncle, na watoto wa kaka yangu,wameungua na moto usiku wa kuamkia leo''Nikki amenukuu ujumbe aliotumiwa leo na Stereo
Bado haijafahamika chanzo cha ajali ya moto huo jitihada za kumtafuta Stereo ziligonga mwamba kutokana na simu yake kutokuwa hewani
Swahili One inampa pole kwa msiba huo

NICK MBISH ATANGAZA KUACHA MUZIKI



Rapper Nikki Mbishi leo ametangaza kuwa ameacha muziki.

Rapper huyo ameelezea uamuzi wake wa kuachana na muziki kutokana na kutokunufaika chochote na kwamba hawezi kuendelea kuwa mtumwa mwa kiwanda cha muziki.
“I’m glad to say I’ve officially decided to quit music….Wishing all the best to the slaves and victims of Music industry,” ametweet rappe huyo. “Nitaziachia tracks zangu zote ambazo hazijatoka for free then SITOINGIA TENA STUDIO kufanya wimbo(MUZIKI BASI).”
“The Industry is designed to frustrate the cats with high degrees of talents and intelligence. Ngwea,Langa,Geez mlale pema wanangu. I will remain as a music fan…and u guys need to find me some hip hop heads to listen to…asanteni,” ameongeza.
“Bora kuwa JAMBAZI kuliko MWANAMUZIKI. Tusije kushikiana bunduki bure maana milango ya kutoka kimaisha ni mingi na muziki ni burudani na biashara sio vita. Industry full of stupid and Illiterate but rich and famous. Mpaka lini tutauza UNGA kwa kivuli cha kuwa WASANII?”





Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga