Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

JOYCE KIRIA AKWAA DENI LA MIL 500 BAADA YA KUTOA SIRI YA MBUNGE WA ZANZIBAR


Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria.
MTANGAZAJI wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria amepokea samansi ya mashtaka kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar, Abdallah Sharia Ameir (CCM) ambaye amedai amlipe fidia ya kumdhalilisha sh. Milioni 500 au amuombe radhi kupitia kipindi chake.
Akiongea, Joyce Kiria alisema kuwa amepokea barua hiyo kwa mikono miwili na anawasubiri wanasheria wake ili waijadili.“Nilimpokea mke wa Mbunge aitwaye Hawa kama mwanamke mwenye matatizo ambaye alifika kutoa sauti yake ili watu wamsaidie mtoto wake mwenye ulemavu.

Baada ya kuongea naye nilimtafuta mheshimiwa ili kumpa nafasi naye aongee ya kwake kama wajibu wangu, lakini cha kushangaza yeye alinikamata na kunipeleka polisi, leo anasema nimemdhalilisha,” alisema Joyce .
Joyce anadaiwa fidia na Mbunge huyo kwa kuitangaza habari ya kumtelekeza mtoto mlemavu ambaye alilepelekwa kwenye kipindi chake na mkewe, Hawa Deusi

KIFO CHA MAMA NTILIE CHASABABISHA VURUGU IRINGA, KITUO CHA POLISI CHACHOMWA MOTO.




Habari kutoka Iringa zinasema kuwa kituo cha polisi cha Ilula mkoani Iringa kimechomwa moto na wananchi wenye hasira kufuatia polisi kumuua mwanamke mmoja mfanyabiashara ya mama ntilie wakati wa msako maalum ulioendeshwa na jeshi la polisi dhidi ya wafanyabiashara na watu wanaokunywa pombe mida ya kazi.
Inasemekana wakati wa purukushani za kukimbia ndipo polisi mmoja alimchota mtama huyo mama wakati anakimbia na kusababisha mama wa watu kuanguka na kufariki dunia hapo hapo.
 
Mabasi ya kwenda mikoani yakiwa yamepaki baada ya wananchi kufunga barabara.

 
Muonekano wa mji wa Ilula mkoani Iringa baada ya wananchi kufunga barabara kuu ya mji huo.


 
Mabasi ya kwenda mikoani yakiwa yamepaki baada ya wananchi kufunga barabara.
 
 
 
 



MKUU WA KITUO CHA POLISI JELA MIAKA 30 KWA UBAKAJI


Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa ya Njombe, imemhukumu aliyekuwa mkuu wa kituo cha Polisi Ilembula kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtuhumiwa aliyekuwa ndani ya mahabusu.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Augustine Rwezile, baada ya mshtakiwa huyo James Nyambenga kukiri kosa hilo mahakamani, ambapo mshakiwa huyo anadaiwa kumtoa msichana huyo kwenye chumba cha mahabusu alikokuwa anashikiliwa na kumbaka.
Mwanamke huyo ambae ni mhudumu wa bar alikuwa anashikiliwa kwenye mahabusu ya kituo hicho kwa tuhuma za uzururaji.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Rwezile amesema ushahidi uliotolewa na upande wa mlalamikaji na vielelezo vya daktari aliyempima msichana huyo viliweza kuithibitishia Mahakama kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo.

MWALIMU MBARONI KWA KUMTUMIKISHA BINTI WA MIAKA 12KUMUUZIA MAYAI NA SOSEJI


MATUKIO ya mateso, unyanyasaji na utumwa kwa watoto yanashika kasi nchini! Safari hii mwalimu wa shule moja ya msingi iliyopo Mburahati jijini Dar aliyetajwa kwa jina moja la Lucy ametia aibu baada ya kutiwa mbaroni katika Kituo cha Polisi cha Magomeni, Dar akituhumiwa kumtumikisha mtoto mwenye umri wa miaka 12 aitwaye Sakina kwa kumuuzisha mayai ya kuchemsha na soseji.

Mwalimu huyo akijitetea juu ya sakata hilo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wetu, tukio hilo lilichukua nafasi maeneo ya Kashuda Bar, Magomeni hivi karibuni baada ya wakazi wa eneo hilo kuhamaki kumuona binti huyo akitembeza mayai na soseji mtaani wakati umri wake ni mdogo kinyume na sheria za ajira.
RAIA WAMZUNGUKA
Ilisemekana kwamba, baada ya kukerwa na kitendo hicho huku Sakina akionekana hana furaha, raia hao wenye hasira kali walimhoji ambapo alimtaja mwalimu huyo kuwa ndiye bosi wake aliyemchukua kutoka Tanga kwa ajili ya kufanya kazi za ndani (hausigeli).
AFUATWA SHULENI
Ilidaiwa kwamba, wakifuatana na mtoto huyo, wakazi hao walifunga safari hadi shuleni kwa mwalimu huyo Mburahati ambapo wanahabari wetu walitonywa na kutia timu hadi kwa mkuu wa shule hiyo, Kibassa ambaye alikiri kuchukizwa na kitendo cha mfanyakazi wake kumwajiri mtoto wa miaka 12 kumtumikisha kazi akiwa ni mwajiri wa serikali.
Mwananfunzi Sakina anayedaiwa kuuzishwa mayai muda wa shule.
“Kimsingi nimesikitishwa kwa sababu Lucy ni mwajiriwa wa serikali, hapaswi kufanya jambo baya kama hili. Kwa umri wake alipaswa awe darasani,” alisema Kibassa.
MWALIMU AJITETEA
Kwa upande wake, Lucy alijitetea kuwa binti huyo aliletewa na mtu aliyemtaja kwa jina la Kizito aliyemuagiza mfanyakazi wa ndani, lakini baada ya kufika binti huyo alimkataa na kudai bado mdogo asingeweza kufanya kazi za ndani.
Mwalimu huyo alisema alikuwa akimsubiri binti mwingine mkubwa aletewe na Kizito ili amrudishe Sakina kwao na kudai kuwa hata biashara ya mayai hakumtuma yeye bali alimtuma John (kijana wake wa kazi) ila inawezekana Sakina alijiingiza kujisaidia na ugumu wa maisha.

Mwalimu huyo akiwekwa kikao.
BINTI ASIMULIA
Akiwa shuleni hapo, mbele ya bosi wake, Sakina alifunguka kuwa amekuwa akifanya biashara hiyo na kufanya kazi za ndani kwa Lucy huku akisimulia kunusurika kubakwa na kupitia mateso mengine kama kunyimwa chakula na kulazimika kutembeza mayai na soseji mchana kutwa.
“Nafanya kazi za ndani na kutembeza mayai, kuna kaka mmoja nilimwomba msaada ili nirudi nyumbani, akanilazimisha tufanye map3nzi ndipo anisaidie, nilipokataa akaniacha,” alisema Sakina.
Hata hivyo, mwalimu huyo alitolewa shuleni hapo chini ya ulinzi mkali kisha kufikishwa Polisi Magomeni katika dawati la jinsia kwa hatua zaidi.

VITA YA U-FIRST LADY IMEANZA, MITANDAO YA KIJAMII YATUMIKA KATIKA KAMPENI


TAYARI imebainika kwamba, baadhi ya viongozi walioonesha nia ya kugombea urais mwaka huu wameanza kupigiwa debe na wake zao ndani ya mitandao ya kijamii ili waume hao watakapoibuka na ushindi wapate nafasi ya ‘u–First Lady’, Risasi Jumamosi linakupa zaidi!
Mama Salma Kikwete.
Taarifa zilizotua juu ya dawati la gazeti hili juzi zilisema kuwa, vita ni nzito kwani baadhi ya wake wa wagombea nao wapo ndani ya mkakati wa kukusanya watu wa kuwaunga mkono waume zao katika kinyang’anyiro hicho kitakachochukua nafasi Oktoba, mwaka huu.
Wakati vita hiyo ikiwa imepamba moto, mnajimu maarufu nchini, Maalim Hassan Hussein naye ameibuka kwenye Risasi Jumamosi na kuanika utabiri mzito juu ya wasifu wa mtu atakayeshinda urais huo.
HALI ILIVYO SASA
Habari zinadai kuwa, baadhi ya wake wa viongozi hao nao wamekuwa wakipita chini kwa chini kukusanya na kuweka sawa makundi ya kisiasa tayari kwa kampeni za kuwaingiza ikulu waume zao.
ISHU NI KUMRITHI MAMA SALAMA KIKWETE
“Kila mke wa mgombea anafanya kampeni za chini kwa chini. Unajua wenyewe kila mmoja anafahamu kwamba ‘mzee’ akiingia ikulu yeye atakuwa First Lady kumrithi wa sasa (mama Salma Kikwete), ndiyo maana siku hizi karibu wake wa wagombea wote wana safari za mikoani kupanga timu ushindi,” kilisema chanzo kimoja.

Mke wa waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa.
FARAJA KOTA YUKO WAZI ZAIDI
Miss Tanzania 2004, Faraja Kota ambaye ni mke wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu aliyetangaza nia, amekuwa akitupia maneno yenye kumpigia kampeni mumewe huyo kwenye Instagram na mitandao mingine ya kijamii.
KWENDA NAYE KANISANI
Desemba mwaka jana, Faraja aliongozana na mumewe huyo ambaye pia ni Mbunge wa Singida Kaskazini kwenda kwenye Kanisa la FPCT, Ilongelo na baadaye kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, Singida ambako mumewe alitangaza rasmi nia yake ya kugombea urais.
MAMA PINDA
Tunu Pinda ni mke wa Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda. Yeye aliwahi kukaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema alishtushwa kusikia habari kwamba, mumewe ametangaza nia ya kugombea urais 2015.
Mke wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
Alisema alipomuuliza mumewe alimwambia hajaita vyombo vya habari kusema hivyo lakini muda ukifika atafanya hivyo. Mama Tunu akasema na yeye anakubaliana na maneno ya mumewe kwamba muda ukifika atangaze kugombea urais.“Kwa hiyo kama alivyosema na iwe hivyo kama Bwana Mungu aishivyo, nasema amina. Kwa sababu muda bado haujafika, utakapofika tutajua,” alisema mama Pinda.
YA MTABIRI SASA
Kuhusu utabiri wa Maalim Hassan, amesema mwaka huu, Tanzania itampata rais wa aina yake kuliko miaka yote iliyopita tangu uhuru (Desemba 9,1961).Akizungumza na gazeti hili Jumatano iliyopita, ofisini kwake, Magomeni, Dar, Maalim Hassan alisema kuwa, rais atakayepatikana mwaka huu atakuwa mtu aliyechanganya dini.
Alisema mtu huyo, kama baba yake atakuwa Muislam basi mama atakuwa Mkristo. Kama mama Muislam, baba itakuwa kinyume cha hapo.
Mke waNaibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli (CCM), January Yusuf Makamba.
TOFAUTI HATA KWA MKE, MUME
Maalim Hassan akaenda mbele zaidi kwa kusema: “Kama wazazi wake wote watakuwa dini moja, basi yeye (mgombea) atakuwa na imani tofauti na mke wake au mume wake (kama kutakuwa na mgombea mwanamke). “Mgombea anaweza kuwa Muislam, kama ni mwanaume basi mke wake atakuwa Muislam. Vivyo hivyo kwa mgombea mwanamke,” alisema Maalim Hassan.
KWA HARAKAHARAKA
Kauli ya Maalim Hassan ina ishara ya kumgusa moja kwa moja, Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli (CCM), January Yusuf Makamba ambaye mama yake mzazi ni Mkristo huku baba yake, mzee Yusuf Makamba akiamini katika Uislam.
WANAOTAJWA KUWANIA URAIS MWAKA HUU
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alitangaza nia hiyo usiku Agosti 22, mwaka jana Ikulu Ndogo ya Jiji la Mwanza.

Margreth Sita.
January Makamba alitangaza nia ya kuwania nafasi hiyo Julai 2, mwaka jana alipokuwa Uingereza katika mkutano wa sekta ya mawasiliano. Wengine ni Mbunge wa Nzega (CCM), Dk. Khamis Andrea Kigwangallah, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Lameck Nchemba (CCM), Waziri Nyalandu (CCM), Mawaziri Wakuu Wastaafu, Frederick Tuluwai Sumaye na Edward Ngoyai Lowassa (wote CCM).
Wengine ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Camillus Membe (CCM), Waziri wa Kilimo na Chakula, Stephen Masatu Wassira na Mbunge wa Sengerema, William Mganga Ngeleja (CCM). Waziri wa Uchukuzi, Samuel John Sitta naye amekuwa akitajwa kujitosa kwenye kijiti cha urais.
Kutoka vyama vya upinzani, ambaye ameshatangazwa na chama chake ni Mwenyekiti wa Cuf, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba. Katibu Mkuu wa Chadema, Wilbroad Peter Slaa yeye amekuwa akigombea kwa chama hicho kwa miaka kumi iliyopita. Lakini kuna tetesi kuwa, huenda Chadema ikamsimisha mwenyekiti wake wa taifa, Freeman Haikaeli Mbowe.

DALALI WA KUWAUZA NA KUWAUA ALBINO APATA STAHIKI YAKE, AUAWA KIKATILI NA WANANCHI.


Tukio hilo lilitokea jana saa saba mchana katika kijiji cha Bulyaheke, kata Bulyaheke, baada ya wananchi kumkamata mtuhumiwa huyo katika kijiji cha Kazunzu na kuwaongoza hadi kijiji cha Bulyaheke kwa mganga huyo.
Wananchi wa vitongoji vya Kazunzu, kijiji cha Nyambemba, kata ya Kazunzu, wakishirikiana na wa kitongoji cha Lueseselo, kata ya Bulyaheke, wamempiga kwa marungu, mawe na mapanga na kisha kumchoma moto mtu ambaye bado hajafahamika, wakimtuhumu kuwa wakala wa kuteka watoto wakiwamo walemavu wa ngozi (albino), akishirikiana na waganga wa kienyeji wapiga ramli kwa imani za kishirikina za kupata utajiri.
Mbali ya kumuua, wananchi hao pia wamevunja na kuchoma moto nyumba 13 zilizoezekwa kwa bati mali ya mganga wa kienyeji mwanamke mpiga ramli mwenye umri wa miaka 40 (jina linahifadhiwa).
Hata hivyo, mganga huyo na familia yake walifanikiwa kuwatoroka wananchi hao.
Tukio hilo lilitokea jana saa saba mchana katika kijiji cha Bulyaheke, kata Bulyaheke, baada ya wananchi kumkamata mtuhumiwa huyo katika kijiji cha Kazunzu na kuwaongoza hadi kijiji cha Bulyaheke kwa mganga huyo.
Richard Mangalamu baba wa mwanafunzi aliyetekwa, Winfrida (11) anayesoma darasa la nne Shule ya Msingi Kazunzu, alisema mtuhumiwa alimwachia mwanafunzi huyo kutokana na kumkuta ana chale mgongoni na kifuani akidai amepoteza ubora.


Mkuu wa Polisi wa Kituo cha Wilaya ya Sengerema, Babu Sanare na Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, Enock Mabula, kwa nyakati tofauti walithibitisha kutokea kwa tukio hilo.


Naye Diwani wa Bulyaheke, Bagadi Nyuki, akiwa eneo la tukio, alisema chanzo cha mauaji hayo ni marehemu kudaiwa kuwa juzi alimteka mwanafunzi wa kike anayesoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Kazunzu na kumvutia vichakani na kisha kumvua nguo na kumpapasa.


Inadaiwa kuwa alimuachia huru baada ya kugundua kuwa hakuwa na sifa zinazohitajika na mganga na mwanafunzi huyo alipofika nyumbani aliwaeleza wazazi wake na ndipo wakishirikiana na wanakijiji wenzao walianza kumsaka mtuhumiwa na kufanikiwa kumtambua.


Inadaiwa baada ya kubanwa mtuhumiwa huyo alikiri na kujitambulisha alikuwa ametoka kijiji cha Katoro, mkoani Geita na alikwenda Sengerema kwa kazi ya uwakala wa kuteka watoto.


Diwani huyo alisema marehemu aliomba apelekwe kijiji jirani cha Bulyaheke umbali wa kilometa sita kutoka Kazunzu kwa mwenyeji wake na mdau mwenzake, Sato, lakini wapofika walikuta amekwisha kutoroka.


Wakati huohuo, mwili wa mtoto Yohana Bahati aliyeuawa kwa kukatwa miguu na mikono, mwili wake utazikwa kesho katika kijiji cha Kataro, mkoani Geita.
CHANZO NIPASHE

BREAKING NEWS :MEZ B AFARIKI DUNIA


Msanii Mez B aka Moses aliyekuwa Mkoani Dodoma kwa matibabu baada ya kurudishwa nyumbani na mama yake amefariki Dunia. Mez B alikuwa akiuguliwa na homa ya mapafu [Pneumonia] na alikuwa kwenye dozi na leo ilikuwa siku ya tatu toka anatumia dawa hizo. 



Leo asubuhi aliamka na kunywa dawa na chakula ila hali yake haikuwa sawa na kuonekana amelegea. Daktari wake alipigiwa siku na kuamuru awekewe drip ila hali yake ikawa mbaya zaidi, wakati wanampeleka hospitalini alifia walipofika mapokezi. Jirana amelezea haya. 

Pole kwa familia ya Mez B, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema, Amen

HALI YA KIKONGWE ALICHAPWA AKIHUSISHWA NA USHIRIKINA BADO NI MBAYA


KIKONGWE Hilda Johnfan Pili (79) aliyepigwa mawe kutokana na imani za kishirikina katika Kijiji cha Kilagano, Peramiho mkoani Ruvuma hivi karibuni, bado hali yake ni mbaya kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata.
Kikongwe akiwa hoi baada ya kupigwa mawe kutokana na imani za kishirikina.
Kikongwe huyo na Maurus Zenda (46) anayedaiwa kuwa ni mwanaye kiukoo, kwa pamoja walijeruhiwa vibaya baada ya kupigwa na baadhi ya ndugu zake kwa kuhisiwa kuhusika katika upotevu wa mtoto Adamu Mselewa (4).
Kwa mujibu wa mmoja wa wanafamilia wa ukoo huo, hali ya bibi huyo bado ni mbaya na wanajitahidi kwa hali na mali kuokoa maisha yake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma alikolazwa.
“Bado hali ni mbaya, bibi bado analalamika maumivu, tunaendelea na matibabu huku tukisubiri madaktari watatueleza nini kuhusu maendeleo yake, ikishindikana hapa tutamhamisha hospitali, afadhali kidogo Maurus,” alisema mwanafamilia huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Mtoto wa kikongwe huyo.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Mihayo Msekhela,  waliwakamata watuhumiwa 10 kutokana na tukio hilo, ambao ni Ambros Mselewa (24) ambaye ni baba mzazi wa mtoto aliyepotea, Maria Zenda (45), Lameck Zenda (22),  Pautas Komba (24), Fredy Mende (24), Gerord Ngonyani (27), Odilo Mwingira (21), Shadrack Ngonyani (22), Hilda Zenda(36) ambao wote ni wakazi wa Kijiji cha Muunganozomba.
Msikhela alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa moja asubuhi baada ya baba mzazi wa mtoto huyo, Ambros Mselewa akiwa pamoja na watu wengine walipoanza kuwashambulia watu hao wakimtaka kijana wao aliyepotea kimauzauza tangu Februari 3, mwaka huu.
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga