Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

KWA NINI MAKAMUZI YA MWANA FA JMOSI YALIFANA HUKO TANGA


Tunajua kuhusu umahiri wake kwenye uandishi wa mashairi pamoja na kumiliki stage, amedumu kwenye game tangu siku ya kwanza na bado anabakia kuwa bora kila siku ndio maana siku ya Jumamosi Oktoba 31, rapa mkongwe, Hamis Corleone Mwinjuma a.k.a Mwana FA aliacha historia ya aina yake Tanga kwenye ile show ya nguvu iliyoandaliwa na Vodacom.
Kabla ya kufanya show hiyo iliyopewa jina la ‘Mcheza Kwao Hutuzwa’ iliyofanyika katika ukumbi wa La Casachika, taarifa kutoka kwenye blog ya Issa Michuzi zimesema Mwana FA alitembelea kituo cha yatima cha Diana kilichopo Tanga na kukabidhi zawadi ya jezi kwa niaba ya kampuni simu ya Vodacom Tanzania.
Mwana FA Tanga
Mwana FA akikabidhi zawadi ya Jezi kwa Niaba ya kampuni ya Vodacom Tanzania kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha Diana, Tanga.
Mbali na hilo, msanii huyo alikabidhi zawadi kwa mshindi wa simu ya Vodafone Smart alipotembelea duka la Vodacom lililopo barabara ya tatu, Tanga.
Mwana FA II
Mwana FA akipiga ‘Selfie’ na mshindi wa Vodafone Smart, Kika Martin Joseph baada ya kumkabidhi zawadi ya simu hiyo kwa niaba ya kampuni ya Vodacom Tanzania.

CHRISS BROWN AFUNGUKA UHUSIANO WAKE ULIOVUNJIKA KWA RIHANNA



Baada ya ukimya wa kama miaka 5 hivi, Chris Brown ameamua kuzungumzia yote yanayomhusu ikiwemo mahusiano yake na Rihanna.
Chris amesema kila kitu ni kama ilikuwa ‘mistake’, na hana haja ya kuwa na majuto kwa kuwa tayari walirekebisha tofauti zao na kwa sasa ‘pepo’ alilonalo ni pepo la kuogopa kushindwa.
Akizungumzia kuhusu yeye na Rihanna, amesema “..naamini ilikuwa ni makosa ambayo siwezi kuyarudia.. nikiangalia nilikuwa nna umri wa kama miaka 17 au 18.. sasa nna 25.. najikuta bado natumikia adhabu ya kufanya huduma za kijamii na natakiwa kuonana na jaji kila baada ya mwezi mmoja na nusu kutokana na tatizo lile..”
Chris Brown na Rihanna walikaa kwenye headlines ambapo imesemekana walijaribu kama kuufufua uhusiano wao, ambapo Chris anasema alihitaji kumuonyesha Rihanna kwamba anaweza kubadilika na kuwa mwanaume ambaye Rihanna anamuhitaji.
Baada ya Chris kumuona Rihanna kwenye show ya Oprah akizungumzia kwa hisia kuhusu Chris, na kusema upo uwezekano wakawa marafiki, Chris aliona namna ambavyo Rihanna anamjali, kitu ambacho hakuwahi kukiona kwa kipindi kirefu, lakini kizaazaa kikawa pale Rihanna alipoanza ‘kutoka’ na Drake ambapo Chris alihisi kuwa Rihanna anafanya hivyo kumuumiza japo yeye hana uadui na yoyote kati yao.
Chris & Drake
“.. Namna ninavyofanya.. Iko wazi.. Hii ni game, sisi ni vijana.. tunafanya hivi ni kwa sababu ya umri. Nadhani tukifikia miaka 30, tutakuwa tumepevuka na malengo yetu hayatokuwa upande huo tena..”
“..Tumalizane na masuala ya ugomvi, itaonyesha namna gani tumekua na tumepevuka..”-Chris Brown

ORODHA YA RAPPERS WANAO ONGOZA KWA KUPULIZA SIGARA ZA WAKUBWA




Kwenye orodha ya wasanii wa kiume wanaofanya muziki wa rapper ambao wanaaminika kuwa wanatumia marijuana sana na huonyesha hata kwenye picha na video zao, hawa watano wapo juu zaidi kwenye orodha hii.
Alchemist
B-Real
Schoolboy Q
Snoop Dogg
Kengete.


SABBY "ANGEL" NDIO USINGIZI WA BOB JUNIOR, AMFUNIKA MKE WA AWALI KWA MAHABA.



MSANII anayechipukia kwa kasi katika anga la filamu Bongo, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ amefunguka kuwa kwa kipindi kifupi ambacho amezama kwenye penzi la staa wa Bongo Fleva, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’, amempa mahaba mazito kiasi cha kumfanya asimkumbuke aliyekuwa mkewe.
Msanii wa filamu Bongo, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ akipozi na 'Bob Junior' kimahaba.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Sabby alisema kuwa ameamua kuonyesha ufundi wake wote wa kimahabati kwa msanii huyo kwani ni mwanaume ambaye amemuona mwenye mapenzi ya dhati.
‘Sabby Angel’ akipozi.
“Sijawahi kukutana na mwanaume mwenye mapenzi kama huyu na mimi zawadi nitakayompa ni mapenzi mazito na nitamaliza ufundi wangu wote kwake na kamwe hatokumbuka kama aliwahi kuwa na mke kabla yangu,” alisema Sabby.Bob Junior aliwahi kumuoa mwigizaji, Halima Ally kisha wakamwagana baada ya kuzaa naye mtoto mmoja.

AUNTY EZEKIEL NA SKENDO YA CHENI YA MILIONI 6




NYOTA wa sinema Bongo, Aunty Ezekiel ameingia matatani na maafande wa Kituo cha Polisi Pangani, Ilala jijini Dar akidaiwa kutokomea na cheni ya Shabani Limo yenye thamani ya shilingi milioni 6.
Nyota wa sinema Bongo, Aunty Ezekiel akiwa Bongo.
Kwa mujibu wa chanzo, mwishoni mwa Februari, mwaka huu, Aunty alikwenda kwa Shabani na kuazima cheni hiyo kwa makubaliano ya kuirejesha baada ya muda jambo ambalo hakulifanya na baadaye, Septemba mwaka huu, akasafiri kwenda Marekani kutangaza utalii wa ndani.
Baada ya kurejea, Oktoba mwaka huu, Shabani alimkomalia Aunty na kufikishana Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar ambapo staa huyo alisema na yeye alimwazima cheni hiyo rafiki yake aitwaye Neema.
Ilidaiwa kuwa, Neema baada ya kubanwa alikiri na kusema aliiweka bondi cheni hiyo na hapo ndipo danadana zilipoanza hivyo jamaa akaamua kwenda kufungua madai mengine Kituo cha Polisi Pangani.
Jumatano iliyopita, mapaparazi wetu walifunga safari mpaka kituoni hapo ambapo baadhi ya askari walikiri kuwepo kwa kesi hiyo lakini waligoma kutoa namba za kumbukumbu za jalada ‘RB’ wakidai mwenye uwezo huo ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova.
Aunty Ezekiel akiwa Marekani alipokwenda kutangaza utalii wa ndani.
“Ni kweli hapa kuna hiyo kesi na ilianzia Oysterbay japo hatuwezi kuitolea maelezo ya kina kwa vile jambo lenyewe limekaa kimapenzi zaidi,” alisema askari mmoja ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake.
Shabani alipotafutwa kwa njia ya simu na kuulizwa juu ya taarifa hizo alisema alimuazima Aunty cheni hiyo ambapo naye alimpa shoga yake.
Aunty alipopatikana na kuulizwa alikana kumfahamu Shabani na kudai hana taarifa zozote za kuwepo kwa ishu hiyo.“Mh! Huo ni uzushi, hakuna kitu kama hicho na wala hizo taarifa sizifahamu, huyo mwanaume simjui ndiyo kwanza namsikia kwako,”alisema Aunty.

ASKOFU GEOR DAVIE AVUNJA NDOA YA SEKRETARI WAKE...



KIMENUKA! Ndoa iliyodumu kwa miaka 15 kati ya Wiston Lotta (52) na Pamella Geofrey (40) imevunjwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kufuatia ushahidi mzito uliotolewa mahakamani hapo kumridhisha Hakimu Hawa Mghuruta.
Askofu Mkuu wa Huduma na Ngurumo ya Upako, George David ‘Geor Davie’.
Askofu Mkuu wa Huduma na Ngurumo ya Upako, George David ‘Geor Davie’ yenye makao makuu yake jijini Arusha ndiye aliyetajwa na mahakama hiyo kuwa ni chanzo cha kuvunjika kwa ndoa hiyo ya Pamella ambaye alikuwa ni sekretari wa kiongozi huyo wa dini baada ya ujumbe mfupi wa maneno (SMS) ukionesha mapenzi kunaswa kwenye simu ya mwanamke huyo ukitokea kwa Geor Davie.
Askofu  Geor Davie akiwa na wasaidizi wake.
Ushahidi uliotolewa na mwanaume ulidai kuwa mgogoro wa ndoa yake ulitokana na mkewe kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Askofu Geor Davie.
Akisoma hukumu ya kesi hiyo Namba 01 ya mwaka 2012, Hakimu Mghuruta alisema kabla ya hukumu, mahakama ilizingatia ushahidi wa mashahidi watano wa upande wa mlalamikaji.Mke wa mtu Pamella Geofrey (katikati) anayedaiwa kutoka kimapenzi na boss wake, Askofu George David ‘Geor Davie’.
Alimtaja mtoto wa kwanza wa wanandoa hao, Sifael Wiston (15) kwamba naye aliieleza mahakama hiyo namna mama yake alivyokuwa akizini nje ya ndoa kwa kukutana na Geor Davie ndani ya gari lake lenye rangi ya silva wakati wa usiku baba yake akiwa safarini.
Mtoto huyo alianika kwamba, walikuwa wakipelekewa juisi na bajia ndani ya gari hilo lenye pazia kisha wao kufunga vioo kwa muda mrefu huku likionekana kutikisika, ushahidi ambao uliwashangaza waumini wa kanisa la askofu huyo.
Askofu George David ‘Geor Davie’ akitoa huduma ya maombezi kwa waumini.
Wiston ambaye alikuwa msaidizi wa Geor Davie, alifungua kesi ya kudai talaka kwa Pamella ili kufikia ukomo wa shauri hilo ambalo lilianza kusikilizwa na Baraza la Usuluhishi wa Ndoa mwaka 2007 lakini ilishindikana kwa vile mkewe alipeleka sababu za uongo kuwa alikuwa akinyanyaswa hivyo kuikimbia nyumba.
Hakimu Mghuruta ameamuru mali zote yakiwemo magari matatu, nyumba iliyopo Sakina na vitu vingine zibaki chini ya mlalamikaji lakini Pamella anaruhusiwa kwenda kuwasalimia watoto wake. Hata hivyo, mahakama ilimtaka Pamella kutowarubuni watoto hao kiasi cha kuathiri masomo yao.

CHEKI VIDEO "SHITOMBE" YA MSANII Y-TONY



CHID BENZI AFUNGUKA KUHUSU KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA



Imekua stori namba 1 kwa mwezi wa October 2014 inayomuhusu msanii kwenye familia ya bongofleva iliyoandikwa au kuripotiwa na kila aina ya chombo cha habari kuanzia TV, Magazeti na hata mitandaoni.

Chidi Benz alikamatwa na dawa za kulevya kete 14 pamoja na bangi kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam akielekea Mbeya kwenye show aliyokua anatakiwa kuifanya kesho yake lakini ilishindikana kutokea baada ya kukamatwa na Polisi, baadae akafikishwa Mahakamani na sasa yuko nje kwa dhamana.

Alipohojiwa na So so fresh ya CloudsFM inayoongozwa na Dj Fetty, haya ni mambo sita aliyoyazungumza ambapo sentensi mbili ni zake na Tour ya Profesa Jay na nyingine nne ni ishu yake ya kukamatwa Airport.
Kuhusu Tour aliyoifanya na Profesa Jay >>> ‘Ilikua poa sana tumezunguka Dodoma, Morogoro na vitongoji vyake… tumekumbuka zamani tulivyokua tukizunguka kijiji baada ya kijiji, tumefanya kazi vizuri sana na Profesa amekua akinisifia kwa kusema nakuona uko poa afya yako iko poa’
‘Aliniambia by the way nilikua nataka kama unaendelea kuvuta, naona mambo ya kuvutavuta umeachana nayo, tunakaa karibia muda wote tunazunguka wote hata kunywa nimesimama kwa hiyo sasa hivi sio tena muda wa kujielezea oooh navuta, oooh sivuti oooh nakunywa…. naendelea na maisha yangu kama kawaida’

Kuhusu kukamatwa Aiport na dawa za kulevya Benz amesema >>> ‘Sikuwaambia Polisi kwamba natumia dawa walizonikamata nazo, niliwaambia dawa nilizokua nazo lazima nilikua nimechanganya kipindi nilikua nazitumia nilikua nafichaficha kwenye nguo zangu, enzi zile nilikua naficha dawa kwa kuziweka hivyo nikiwa sitaki mtu ajue’
‘Shetta aliponipigia simu ya fasta ili tusafiri kutoka Dar es salaam kwa ndege mpaka Mbeya nikalichukua tu shati na kulivaa na jeans na nilivyofika Airport nikawa namtania tu Shetta namwambia mdogo wangu nimebeba mambo kibao, mabegi yamejaa yote ila sina viatu wala nguo, imagine nafika pale nasachiwa nakutwa na dawa kwenye mfuko wa shati kushoto… sio kama nimeficha au nini’

‘Sio kitu nilikua nimepanga, sio kitu nilikua nimeplan…. mi mwenyewe nimejisachi nikakutwa nayo, sijakamatwa…… mimi nimezitoa…. natoa hivi nakutana na vidude kama kadhaa naviona tu mkononi hapa, jamaa akaviona akaniambia hii nini? nikamwambia hii dawa lakini sijui imekuaje na mimi pale kidogo kibinadamu akili ilikua imeniruka kugundua ile ni dawa na nimeitoa mwenyewe’

‘Kama nilipigwa na butwaa hivi nikajaribu kuomba jamaa nikawaambia bwana sorry kuna time nilikua natumia hizi vitu nikaachana nazo, so kama mnaweza kunielewa mkanisamehe wakasema hakuna….. wakasachi kila begi na hawakukuta kitu kingine’ – Chidi Benz
Kesi ya Chidi Benz imepangwa tena November 11 2014.


javascript://

MSANII WA BONGO MOVIE AFARIKI DUNIA



Muigizaji Mzee Manento amefariki dunia usiku wa kuamkia jana.
Mzee Mnento atakumbukwa hasa kwa filamu alizocheza kiumakin na marehemu Kanumba  ambazo  ni Hero of the church, Dar to lagos,fake pastor n.k.
Mungu ailaze Roho ya maerehemu mahali pema peponi amina.

HAYA NDO MACHACHE YA HAMISA MOBETO....



Hamisa Hassani Mobeto amezaliwa mwaka 1994 mkoani Mwanza na kabila
lake ni Mnyamwezi. Mwanzo wake katika tasnia ya u-miss na modelling
ilianza baada ya hamisa kuibuka mshindi wa shindano la  Miss XXL BACK TO
SCHOOL BASH  Mwaka 2010 iliyoandaliwa na kipindi cha XXL kutoka Clouds
Fm. Mwaka 2011 Hamisa alishiriki mashindano ya Miss Dar Indian Ocean na
alifanikiwa kushika nafasi ya pili , pia mwaka huohuo alikua mshindi wa
pili wa miss kinondoni na kufanikiwa kuingia kwenye Nusu fainali ya miss
Tanzania.
Hamisa-Mobeto-slide--vibe-co-tz
Mwaka 2012 hamisa alishiriki kwenye mashindano ya Miss Univeristy Afrika na kuingia hatua ya 10 bora.
hamisa-1
Kutokea Hapo hamisa amekuwa gumzo kwenye tasnia ya uanamitindo na
filamu pia. Pia amisa ni video vixen na wengi mnaweza kumuona kwenye
video ya Quick Rocka ya My Baby. Mwaka 2014  Hamisa alitokea  kwenye
cover page la Pulse Magazine la Nchini Kenya.
hamisa Cover
Akiwa Ndio kwanza ana miaka 21 Hamisa ni mtu wa kuangaliwa sana sababu anategemewa kufanya mambo makubwa zaidi.

MOTO WAMUWAKIA MISS TANZANIA 2014



WAKATI serikali kupita Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), ikisema itakifuta cheti cha kuzaliwa cha Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu, taarifa zinasema kwamba hawezi tena kuendelea na taji hilo.
FikraPevu imethibitisha kwamba uamuzi umekwisha kufanyika wa kumvua Sitti taji hilo alilovikwa katika mazingira tata, uamuzi unaotarajiwa kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa.
Hata hivyo, haijafahamika kama hatua hiyo itachukuliwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) ama Sitti mwenyewe baada ya kubainika kwamba taji hilo linazidi kuiweka pabaya familia ya Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, ambaye ni baba yake.
Uchunguzi wa FikraPevu umebaini kwamba hata hatua ya awali ya kuwania taji hilo ilichukuliwa na Sitti na baadhi ya wanafamilia bila kushirikishwa kwa Mbunge Mtemvu, jambo ambalo lilimsononesha awali katika ushiriki wa Miss Temeke.
FikraPevu imefahamishwa kwamba Mbunge Mtemvu amekerwa na hali inayoendelea ikiwa ni pamoja na kuwapo utata wa cheti cha kuzaliwa cha mwanae Sitti, pamoja na kuwa anawajibika kisheria kwa anayoyafanya kutokana na kufikia umri wa zaidi ya miaka 18.
Kwa upande wake, RITA imesema inaweza kukifuta cheti kilichotolewa Temeke na kuchukua hatua stahiki ikibainika kwamba alitoa taarifa za uongo wakati wa kuwasilisha maombi ya kukupata cheti hicho.
Mtendaji Mkuu wa RITA, Philip Saliboko, ameiambia FikraPevu leo Alhamisi Oktoba 31, 2014 kwamba kwa sasa wanakamilisha uchunguzi wa kina kuhusiana na cheti hicho, baada ya kuibuka utata wa taarifa za kuwapo vyeti viwili vinavyotofautiana mwaka wa kuzaliwa.
Unaweza soma  
Baada ya kuibuka kwa utata huo, RITA ilianza upekuzi maalumu wa nyaraka alizowasilisha Sitti katika ofisi za RITA Temeke ili kubaini kwanza uhalali wa cheti, kabla ya kutafuta ukweli wa taarifa zilizowasilishwa chini ya kiapo.

NAY APATA MTOTO WA KIUME NA SIWEMA


Rapper Nay Wa Mitego na mchumba wake Siwema wamebarikiwa kupata mtoto wa kiume tarehe 28/10/2014 ambaye ni siku ya kuzaliwa ya mama mzazi wa Ney Wa Mitego.

DIAMOND PLATINUMZ NA WEMA SEPETU WAPIGANA CHINI?!!




Pamoja na kujishaua mbele ya kamera za wanahabari na simu za kuteleza (smart phones) kisha kutupia kwenye mitandao ya kijamii wakizuga wapo pamoja, habari ya mjini inadai kwamba, s3xy lady wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ amemmwaga staa wa Ngoma ya Mdogomdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni rafiki mkubwa wa wapenzi hao, ishu ya kumwagana ilikuwepo muda mrefu lakini kinachoendelea ni kuwazuga mashabiki wao ili wasishuke kisanaa.
Chanzo hicho kilifunguka kwamba, siku chache zilizopita Wema au Madam kama anavyopenda kuitwa, alimwambia Diamond kuwa anakwenda China kuchukua mzigo bila kumwambia ni mzigo gani na kwamba huko aliambatana na wanaume wanne, wawili wakiwa ni Martin Kadinda na Petit Man.
Ilidaiwa kwamba wanaume wengine wawili wapo kwenye mabano, jambo ambalo Diamond au Dangote kama anavyopenda kujiita, hakuliafiki suala hilo lakini Madam akasema liwalo na liwe yaani kama ‘mbwai iwe mbwai’ hivyo akampuuza na kwenda zake China!
Chanzo hicho kilidai kwamba, kuna wakati Madam alimuomba Dangote au Chibu ampe fedha kwa ajili ya mtaji ambapo jamaa huyo alikubali lakini siku zikawa zinayoyoma bila dalili hivyo Wema akaona wa nini kama mtu mwenyewe hawezi kumsaidia?
Ilisemekana kwamba, baada ya kuona hali hiyo, Wema alijiongeza na kuanza kukubaliana na makelele mengi kuwa jamaa huyo anamtumia kibiashara huku yeye akilamba shoo na kupiga fedha ndefu ndani na nje ya Bongo.
Chanzo hicho kiliendelea kumwaga ‘ubuyu’ kwamba, tabia ya Diamond ya ubahili, nayo imechangia kwa Wema kukaa pembeni kwani jamaa huyo siyo mkataji wa mkwanja kama ilivyokuwa kwa yule kigogo wa Wema, Clement.
“Wewe unamuonaje Wema? Yule mtoto bei mbaya bwana. Matunzo yake si mchezo. Sasa Dangote na ubahili wake ndiyo hivyo atamsikia Madam kwenye bomba,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho kilitiririka: “Unalikumbuka lile BMW (gari) alilodaiwa Wema kapewa na Kadinda siku ya bethidei yake? Unajua Diamond alikuwa Marekani, sasa aliporudi akataka kujua BMW imetoka wapi maana yeye alitoa Murano, hapo ndipo moto ukawaka na wakawa hawaivani tena.”
Habari ziliendelea kupeperushwa kwamba siku ya bethidei ya Diamond ambapo jamaa huyo alizawadiwa BMW X6 na uongozi wake wa Wasafi, Wema alikwenda kwenye shughuli tu ili kuonekana kwenye kamera.
Ilisemekana kwamba, ndiyo maana kwenye shughuli hiyo Diamond ndiye aliyekuwa akihaha kuhakikisha Wema hapati usumbufu tofauti na Wema aliyekuwa anafuata tu maelekezo ‘kishingo upande’ kwani ndani yake hakuna mapenz tena.
Ilisemekana kwamba, baada ya tukio lile kulipita ukimya fulani huku kila mmoja akiishi kwake tofauti na awali ambapo Diamond alikuwa akijinasibu kuwa huwa analala nyumbani kwa baby (Wema), Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar.
Kwenye bethidei ya mwigizaji ambaye ni shosti wa Wema, Aunty Ezekiel, Diamond ndiye alikuwa wa kwanza kuingia ukumbini kwenye Mgahawa wa Rodizio uliopo Masaki jijini Dar, huku kukiwa na taarifa kwamba Madam asingekuwepo kwa kuwa alikuwa safarini.
Wakati shughuli ikiendelea, Diamond alionekana mwenye furaha akiwa na timu yake lakini ghafla alipoibuka Wema upepo ukabadilika.
Wema alipoingia ukumbini akitokea safarini hata kabla ya kwenda nyumbani, alimpita Diamond, akaenda kusalimiana na Aunty kisha akaanza kuzunguka kwenye meza kusalimiana na mtu mmojammoja, cha ajabu alipofika upande aliokuwa ameketi Diamond na timu yake, aliwaruka na kwenda moja kwa moja kusalimiana na mwigizaji Jacqueline Wolper Massawe.
Ishu hiyo iliibua minong’ono kila kona ya ukumbi huo na kuthibitisha zile tetesi kwamba hawapo kwenye uhusiano mzuri.Wakati Wema akifanya yake na Aunty, Diamond alipishana naye kama hawajuani na kukimbilia kwenye gari akiwa na timu yake tayari kwa kutimua.
Mwanahabari wetu alipotaka kujua kwa nini Diamond na ‘kruu’ yake waliacha sherehe wakitaka kutimua, mmoja wa memba wa timu yake ya Wasafi alisikika akisema ‘huyu demu siyo, hata ungekuwa wewe ingekuuma. Jambo alilomtendea mshikaji siyo poa kabisa’.
Alipododoswa Wema juu ya kuzama kwake ukumbini na kumfanya Diamond achomoke bila ya kusalimiana alishindwa kutoa majibu ya kina na kusema hakujua nini kilimkimbiza ila yeye alikuwa pale kwa ajili bethidei ya Aunt na si kingine.
Alipofuatwa Diamond kuzungumzia juu ya kutoka nduki baada ya Wema kuingia ukumbini hapo, aliomba mwandishi wetu amwache kwa maana kwamba ampotezee na kuzama kwenye ndinga lake na kuondoka kwa mbwembwe.
Hata kesho yake alipotafutwa kwenye simu yake ya mkononi ili aweze kuzungumzia hilo hakuonesha ushirikiano kwani simu yake ya kiganjani haikupokelewa muda wote alipopigiwa.
Penzi la Wema na Diamond limekuwa likigubikwa na sarakasi nyingi kila kukicha.
Wawili hao waliwahi kumwagana kipindi cha nyuma kisha kurudiana Oktoba, mwaka jana. Kabla ya kurudiana, kijiti cha penz la Diamond kilikuwa kikishikiliwa na Mtangazaji Penniel Mungilwa ‘Penny’ huku cha Wema kikiwa kwa yule kigogo wake, Clement.
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga