Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

Madawa ya Kulevya yampeleka Mbunge wa Kinondoni,Iddi Azzan Polisi.

-->
KUFUATIA kutupiwa skendo za kuhusika na usafirishaji wa madawa ya kulevya nje ya nchi, Mbunge wa Kinondoni jijini Dar, Idd Azzan ametinga polisi Julai 29, mwaka huu na kuwataka wamchunguze kwa kina.

Madawa ya kulevya.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Idd Azzan alifika katika Kituo Kikuu cha Polisi Posta jijini Dar na kukutana na Kamanda wa Kanda Maalumu, Kamishna, Suleiman Kova.
“Kikubwa Azzan amemwambia Kova kwamba anataka jeshi la polisi limchunguze na kisha liwaambie wananchi kama yeye anahusika na biashara hiyo au la,” kimesema chanzo chetu.
Baada ya kupata habari hizo, Risasi Mchanganyiko lilimpigia simu Azzan ambaye alikiri kufika polisi na kuwataka wamchunguze kwa kina.

Mbunge wa Kinondoni jijini Dar, Idd Azzan.
“Kila kinapofika kipindi kama hiki huwa kuna vuguvugu la uchaguzi, hivyo maneno kama haya husemwa ili kuharibiana sifa, nimewataka polisi wanichunguze na watakachokipata watoe taarifa kwa wananchi,” alisema.
Hivi karibuni Mbunge huyo alitajwa katika habari zilizosambazwa mtandaoni kwamba anahusika na biashara hiyo baada ya mfungwa mmoja wa gereza moja nchini Hong Kong kumtaja kwamba ndiye anayewatuma vijana nje ya nchi kupeleka madawa ya kulevya.
Hata hivyo, Mbunge huyo amekanusha taarifa hizo kwa kusema kuwa hausiki kwa njia moja ama nyingine na kutaka mfungwa huyo atajwe jina lake kamili, namba yake ya ufungwa na hata ndugu zake waliopo hapa nchini ili ukweli ujulikane.
Barua zilizosambazwa mtandaoni ambapo jina la Mhe. Idd Azzan lilitajwa kuhusika na dawa za kulevya:




Source:GPL

Ajali!!!!Akuta Panya Ndani ya Wali Rost Nyama Aliouagiza.


Hali ya Sitofahamu imejitokeza katika Mgahawa mmoja huko Africa Magharibu baada ya Mteja aliyekuwa ameagiza Wali Rost nyama ya kukaanga kukutana na "KAPANYA" Kadogo kameiva ndani ya chakula alichokiagiza.

Mteja huyo alikumbwa na bumbuwazi na hasa ukizingatia alikuwa ameshakula chakula hicho kwa zaidi ya Asilimia 90.

Kutolewa kwa Nando BBA,Furaha kwa Raia wa Ghana


Watu tofauti tofauti wamekuwa wakitoa maoni yao katika mitandao mbali mbali ya kijamii kuhusiana na Mtazamo wao juu ya kutolewa kwa Mshiriki kutoka Tanzania Nando katika jumba la BBA The Chase.

Nando alitolewa mara baada ya kikao cha dharula kilichomwita kumjulisha kuhusu makosa yake ambayo yalikuwa yanahatarisha mwenendo mzima wa BBA The Chase hasa baada ya kumpiga kibao mshiriki mwenzake, Elikem na kumtishia kumchoma kisu.

Furaha zaidi ni kwa mashabiki kutoka nchini Ghana ambao walipatwa na hasira baada ya Nando kumdhalilisha mshiriki kutoka nchi hiyo aliyeondolewa wiki 2 zilizopita.

Angalia Alichokiandika Selly katika Ukurasa wa Twitter Baada ya Nando Kutimuliwa BBA The Chase.

-->   Mshiriki kutoka Ghana aliyewahi kukashifiwa ya kwamba amemwambukiza magonjwa ya zinaa mshiriki wa Tanzania, Selly ameandika Kauli ya Kufurahia kutolewa kwa Nando katika Jumba hilo la BBA.

Angalia Mwenyewe:-


@therealsellygh
My God has fought my battle! All the stigmatization..hmm!! Fanx 2 all my friends and fans! Fanks to Africa!!

 

Za mwizi, 40.!!! Kibaka achezea kipigo huko Kawe, ni baada ya kuruka geti.


Mtuhumiwa wa wizi akiomba kusamehewa wakati mtu mwenye hasira kali akijiandaa kumtupia tofali kichwani ambalo lilimjeruhi vibaya mtuhumiwa huyo.
Mwananchi mwenye hasira akimsulubu mtuhumiwa huyo kwa teke.…
Mtuhumiwa wa wizi akiomba kusamehewa wakati mtu mwenye hasira kali akijiandaa kumtupia tofali kichwani ambalo lilimjeruhi vibaya mtuhumiwa huyo.
Mwananchi mwenye hasira akimsulubu mtuhumiwa huyo kwa teke.
Akisulubiwa kwa bakora na mmoja wa wananchi waliochoshwa na wizi.
...Akiendelea kusulubiwa kabla ya kupelekwa polisi.
Baada ya kulainika akawa anapelekwa polisi.
Kutokana na kipigo jamaa huyo alianguka hatua iliyofanya watu hao wenye hasira kutawanyika eneo la tukio, wakidhani mtuhumiwa amekufa.

MTU mmoja aliyetuhumiwa kuwa ni mwizi amenusurika kufa baada ya kundi la wananchi kumpa kipigo cha maana, leo mchana katika eneo la Mbezi-Darajani, Kawe mjini Dar es Salaam. Mtu huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja inadaiwa alikutwa akiruka geti kuingia ndani kwenye nyumba ya mkazi moja wa eneo hilo. Picha zifuatazo ni baadhi ya matukio wakati mtuhumiwa huyo alipokuwa akipata kichapo hicho. (Picha zote na Bashir Nkoromo)

Source:GPL

Ndege Abadilika na kuwa Binadamu baada ya Kudondoka Chini Mchana Kweupee!!!

-->

Walioshuhudia tukio hilo wamesema ilikuwa kama sinema au mchezo wa kuigiza kwani walikuwa ndege watatu wanapaa angani, ghafla mmoja akadondoka na akatumbukia katika ki mfereji cha maji, hapo ndipo alipojaza watu kwani alibadilika kutoka kuwa ndege na kuwa binadamu.

Ilibidi polisi waingilie kati na kumchukua mwanamke huyo ambaye alijieleza ya kwamba anatokea Ikole na Ni Mkazi wa Jimbo hilo la Ekiti Huko Nigeria.

Polisi hawaamini uchawi, sijui suala la mwanamke huyo watalishughulikiaje!!!!

Justin Bieber Awatemea Mate Mashabiki walikuwa wamejazana kumshangaa!!!


Kweli majuu hapaishiwi vituko, Mkali wa Pop Kijana mwenye asili ya Canada, Justin Bieber amefanya Kufuru ya aina yake baada ya kuwatemea mate mamia ya mashabiki waliokuwa wamejazana chini katika ghoroma moja alipokuwa amekwenda kwa rafiki zake Alhamis ya Tarehe 25 July. Angalia Picha zaidi Chini..

Mwangalie Shakira, Alivyoji shape baada ya Kuzaa!!!


 

Siku chache zilizopita Msanii mzaliwa wa Columbia, Shakira alikutwa akijiachia na ka Bikini Ikiwa ni Miezi 6 tu baada ya kujifungua mtoto wake wa kwanza. Shakira, 36, amefanya kazi kubwa kuurudisha mwili wake baada ya muda mfupi hasa ukizingatia na umri alionao na kujifungua kwake.

Picha hizo zimepigwa akiwa mapumzikoni huko Hawaii.


photophoto

Maskini, Msichana wa Chuo Akutwa Amefariki katika Nyumba ya Kulala Wageni.





Msichana Aliyetambuliwa kwa jina la Florence Ngwu, Mwanafunzi katika chuo kikuu cha Nigeria Amepatwa na Umauti Katika Hotel Moja Mjini Lagos, Nigeria. Mwili wa Msichana Huyo Ulikutwa sakafuni.

Mpaka Sasa hakuna taarifa za ziada zilizotolewa, pia haijajulikana ni kitu gani kilimtoa Chuoni na Kwenda Lagos.


Rafiki Wa Sharo Milionea Adaiwa Kudhulumu Mali za Marehemu

-->


MALI zilizoachwa na aliyekuwa staa wa vichekesho Bongo, marehemu Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Milionea’ zinadaiwa kudhulumiwa na rafiki yake wa karibu aliyejulikana kwa jina moja la Suma, Risasi Jumamosi lina  mkanda wote.


MADAI
Chanzo chetu kilichoongea na gazeti hili Julai 25, mwaka huu kilisema Suma anadaiwa kudhulumu mali za Sharo kufuatia kupewa madaraka ya kufuatilia na kuuza baadhi ya vitu bila fedha kumfikia mama wa marehemu, Zainabu Mkieti.

MAMA WA SHARO AFUNGUKA
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu Alhamisi iliyopita, mama huyo alikiri kuonekana kwa njama za Suma kudhulumu mali hizo likiwemo gari aina ya Opa lenye namba za usajili T 879 CAR na shilingi milioni 1. 2 za seti ya sofa alizonunua marehemu siku chache kabla ya kifo.

AZUNGUMZIA GARI
“Kweli nahitaji msaada ili nifanikishe kupata mali za mwanangu kwani kuna mambo hayaeleweki, kikubwa ni gari ambalo baada ya arobaini tulimpa Suma akaliuze kwa shilingi milioni kumi na moja na anipe fedha hizo lakini hadi sasa sijaona hata shilingi mia. Arobaini ya Sharo ilikuwa Januari 2013.

FEDHA ZA MASOFA
“Ukiachilia mbali gari, kuna fedha za masofa shilingi milioni moja na laki mbili sijazipata hadi leo, Suma aliahidi kunipa baada ya kuuza masofa hayo kwa dada yake na nimeshajaribu kuzungumza naye lakini hakuna majibu ya ukweli.
“Kabla ya Tuzo za Kili Music, Juni, mwaka huu, mimi nilikuja Dar na nikaongea na Suma na mama yake kuhusu fedha hizo, nilipomuuliza kuhusu gari, Suma akasema hataliuza na badala yake baada ya siku mbili angenitumia fedha lakini hadi leo hii simpati kwenye simu.

FEDHA ZILIKUWA ZITUMIKE KWA UJENZI
“Nakosa njia rahisi ya kuzipata fedha hizo maana huyu Suma naona kama mjanja, nilikuwa nataka kuanza ujenzi  wa nyumba kwenye kiwanja alichokiacha marehemu lakini naona kama muda unakwenda,” alisema mama mzazi wa Sharo.

MAJIBU YA SUMA
Suma baada ya kupatikana kwenye simu yake ya kiganjani na kusomewa mashitaka hayo, alidai ameshaongea na mama Sharo lakini alisafiri na ni kweli alikuwa hapatikani kwenye simu.
“Mbona nimeshaongea na mama na mambo tumeyaweka safi, ujue nilikuwa South Africa (Afrika Kusini) nina kama wiki tatu tangu nirudi na kusema kweli sijawasiliana na mama Sharo ila tutamalizana tu mambo yakiwa vizuri,” alisema Suma.

KUMBUKUMBU
Sharo Milionea alifariki dunia kwa ajali ya barabarani Novemba 19, 2012 iliyotokea kwenye Kijiji cha Songa Maguzoni, Muheza Tanga akiwa ndani ya gari aina ya Harrier lenye namba za usajili T 378 BVR likitokea Dar es Salaam kwenda Tanga.
Alizikwa Novemba 23 kijijini kwao, Lusanga, Muheza, Tanga.

Source: GPL

Angalia Jinsi Bongo Movie Wanavyopondwa na Kutathminiwa hapa



UTAJUAJE NI BONGO MOVIE? 

1.Jini akifika barabarani
anaangalia
pande zote ndo avuke barabara. 

2. Matajiri majumba yao yana askari
badala ya electric
fence &
gates.
3.Trailer inachukua
dakika 40.
4.Part2 ya movie ukiiona
mwanzo unajua part1
ilikuwaje.
5.Madem wanaamka wanamake ups
usoni na hereni kabisa.
6.Wakifika hotelini imezoeleka ni juice
inaagizwa au wine
isiyofunguliwa.
7.Nusu saa mtu anatembea,anafanya
mazoezi,anakimbizwa au ananunua vitu.
8.Wimbo wa malavidavi
unaimba
mpaka unaisha.
9.Mtu yupo
village,life gumu ana wave kichwani.
10.Wote wanaouwawa kwa risasi
hupigwa kifuani au
tumboni sio kichwani.
11.Jambazi
lazima awe anavaa miwani nyeusi,koti
kubwa na mvuta sigara mwenye sauti
nene na sura ya kutisha
12Tajiri anakuja kumpenda maskini.
13. Jina La Movie La Kingereza, Ndani
Mazungumzo Ni Kwa Kiswahili.
14.Editor Roy Kijusi, Camera man
Inosenti Kijusi, graphic designer Roy
Kijusi, Location manager Happy Kijusi,
Mavazi Suzy Kijusi.
15.Movie inapart1 na part2,lakn
ukiangalia unagundua ni disc.1 na disc.2
16.movie inaitwa life is harder (mfano)
afu kwenye kava watu wameweka
mapozi ya mamodo na warembo."


Hii nimeikuta face book, huku ikipata Comment zaidi ya 30, Likes ndo Usiseme, Vipi ndugu Msomaji wangu, unalionaje hili?

Wizi wa Rasilimali za Nchi wamkosesha Amani Dk Slaa.


Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Chadema,Dk Willibrod Slaa amesema Tanzania haiwezi kuendelea kuwa na amani kama wizi wa rasilimali za taifa utaendelea.
Dk Slaa aliyasema hayo Dar es Salaam jana, wakati alipofungua mkutano wa Bodi ya Kimataifa ya Shirikisho la Vyama vya Kidemokrasia kwa Vijana (IYDU) ambao unafanyika kwa mara ya kwanza katika nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara.
“Amani inakuwapo mahali penye haki” alisema Dk Slaa na kutolea mfano wa askari ambao wamekuwa wakikamatwa na nyara za taifa wakati wao ni vyombo vya dola, huku pia akisema migogoro ya ardhi inayokithiri inaweka rehani amani ya taifa hili.
Haki nyingine alizolalamilia Dk Slaa ni pamoja na kuminywa kwa demokrasia ambapo ametolea mfano wa polisi kuzuia mikutano ya Chadema huku akiwatuhumu kuwa wamekuwa mashabiki wa siasa badala ya kutimiza wajibu wa kulinda amani kwenye mikutano hiyo.
Kuhusu msajili wa vyama vya siasa John Tendwa, Dk Slaa alisema Chadema walishamfuta kwenye orodha ya watu wanaowasiliana nao.
Akizungumzia mpango wa chama hicho kuanzisha kikosi cha ulinzi, Katibu huyo alisema hata kwenye majumba ya kawaida watu wanakuwa na walinzi wao iweje wao kama chama wasifanye hivyo.
“Kuna walinzi wengi tu wanalinda majumba ya watu mjini, ni sheria gani inayotukataza sisi?” alihoji Dk Slaa.
Kwa upande wa ajira alisema, hakuna nchi inayoweza kuwa na uchumi imara kama vijana wake hawana ajira. Naye Mwenyekiti wa IYDU, Aris Kalafatis alisema ujumbe wao mkubwa kwa vijana wa Tanzania ni kutaka mabadiliko hususan katika masuala ya maendeleo,huduma za jamii na ukosefu wa ajira.
Akizungumzia migogoro mingine inayotokea katika mataifa kama Misri na Tunisia, Kalafatis alisema hawaungi mkono kudai haki kwa njia za machafuko, wanachohitaji ni kuona migogoro inatatuliwa kwa njia za mazungumzo na siyo kama hali ilivyo sasa.


Chanzo: Mwananchi

Nabii Achezea Kipacho, Baada ya Kutuhumiwa kuwa na Uhusiano na Mume wa Mtu, Mchungaji.

-->
Nabii Juliana Aliyechezea Kichapo

Stori:Gladness Mallya na Sanchawa
MWANAMKE anayejulikana kwa jina la Nabii Juliana wa Kanisa la Miracle Assemblies of God, amepigwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kudaiwa kuingilia ndoa ya Mchungaji Richard Kiondo.

Nabii Juliana Aliyechezea Kichapo
Tukio hilo la aina yake ambalo lilikusanya umati wa watu, lilitokea hivi karibuni maeneo ya Ukonga Mazizini, jijini Dar ambapo nabii huyo alipigwa hadi kuchaniwa nguo.
Akielezea mkasa huo, mtoto wa mchungaji wa kanisa hilo, Christina Kiondo alisema baba yake alikuwa akishirikiana kwa huduma ya kanisa na Nabii Juliana lakini katika ushirika huo anaamini wawili hao walikuwa na uhusiano usiofaa.
Alisema kisa cha nabii huyo kupigwa, hivi karibuni mwanamke mmoja alikwenda nyumbani kwa Mchungaji Kiondo na kuwaeleza watoto hao kwamba anamdai baba yao shilingi 40,000, kitu ambacho kiliwashitua sana kwa kuwa baba yao anaishi kwa nabii na pia hawakujua fedha hizo alikopa kwa ajili ya familia gani.
Mtoto mkubwa wa mchungaji huyo, alimtuma mdogo wake nyumbani kwa nabii huyo kwa lengo la kwenda kumuita baba yao ili aje kuzungumza na mwanamke huyo.
Ilidaiwa kuwa, mtoto huyo alipofika alikutana na nabii na kumwambia amemfuata baba yake lakini alimfukuza.
“Baadaye alikuja hapa nyumbani na kuanzisha varangati kitu ambacho hakikukubalika kwa majirani kwani tangu siku nyingi wanajua uhusiano wake wa baba.
“Majirani walitoka kwa wingi baada ya kumsikia nabii akitufanyia fujo, walianza kumshushia kipigo mpaka alipokuja kuokolewa na mjumbe wa eneo hili na kupelekwa polisi,” alisema Christina.
Akizungumza na mapaparazi wetu, mjumbe wa eneo hilo Joseph John ‘Mzee Kasheshe’ alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Kwa upande wake, mke halali wa mchungaji huo ambaye yuko Mbagala kwa matibabu, alisema alizipata taarifa za nabii huyo kupigwa.
Aliongeza kuwa tangu zamani mama huyo alikuwa akienda na mumewe nyumbani hapo akidhani kuwa wote ni watumishi wa Mungu hivyo hakuwahi kuwatilia shaka hadi baadaye sana aliponyetishiwa na watu.
Kufuatia kipigo hicho, Nabii Juliana alipofika polisi alitoa malalamiko yake na kufungua kesi yenye kumbukumbu: MAZ/RB/2246/2013 KUHARIBU MALI.

Source: GPL.

Mwanafunzi Ashikiwa Uchawi, Akutwa na zana kibao za uchawi huku akiwa na Nguo ya Ndani Tu!!!


Stori:Gladness Mallya na Haruni Sanchawa
AMINI usiamini, duniani kuna uchawi! Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Pasco (21) ambaye pia ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Samaritan iliyopo wilayani Rorya mkoani Mara amekutwa getini kwa kaka’ke, Edward Raphael akiwa amefungwa kamba na matunguri.
Denti akiwa amaefungwa kamba
Tukio hilo lilijiri hivi karibuni huko Yombo-Buza jijini Dar na kuibua sekeseke la aina yake kutokana na mazagazaga ya kichawi aliyokutwa nayo.
Kwa mujibu wa mashuhuda, Pasco alikuwa amefungwa kamba mikononi na miguuni huku akiwa na nguo ya ndani pekee.
Habari zilieleza kuwa pia kijana huyo alikuwa amepakwa unga na kuandikwa maandishi ya Kiarabu mwilini huku kiunoni akiwa na shanga, hali iliyowashangaza wengi.
Polisi akiwa eneo la tukio
Akizungumza na wanahabari wetu juu ya tukio hilo, kaka wa kijana huyo alisema tukio hilo lilitokea siku ya Jumapili, wiki mbili zilizopita ambapo aliamka na kujiandaa kwa ajili ya kwenda kwenye shughuli zake lakini alipofungua geti alishangaa kumuona mtu akiwa amelala akiwa hajitambui.
Alisema baada ya tukio hilo, alirudi ndani haraka na kumwita mpangaji wake ili akashuhudie alichokiona.

Mazagazaga aliyo kutwa nayo
Alisimulia kuwa baada ya mpangaji huyo kuamka, waliamua kwenda polisi lakini wakiwa huko, mkewe aliamua kwenda kumchunguza mtu huyo kwa makini usoni ambapo aligundua kuwa ni shemeji yake, jambo ambalo lilizidi kuwachanganya watu.
Alisema aliporudi alikuta umati mkubwa wa watu umemzunguka Pasco.
Wakazi wa eneo hilo wakishangaa

Kaka mtu alisema kuwa alitimba na askari ambao walimfungua kamba na safari ya kuelekea kituo cha polisi ikaanza lakini wakiwa njiani, kijana huyo alikuwa akiongea maneno ya ajabu kama vile mtu mwenye majini.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Nyumba Kumi, Shina la Mube, Joseph Paja alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema naye alikuwa miongoni mwa mashuhuda.
Alisema kuwa alipofika, alikuta kijana huyo aliyewahi kuishi mtaani hapo kwa kipindi kirefu akiwa amefungwa kamba miguuni na mikononi, hali ambayo ilimshangaza kila mtu.
Mchungaji wa Kanisa la Church of World, Steven Paul ambaye naye alishuhudia tukio hilo, alisema kuwa baada ya ndugu kuamua kumpeleka polisi aliambatana nao hadi kituoni lakini walipofika, askari walimtema kwa kigezo kuwa hakuwa na kesi ya kufunguliwa, wakashauri apelekwe hospitali.
Ilielezwa kuwa zoezi la kumpeleka hospitali lilifanyika lakini walipofika huko, madaktari walimkataa kwa kigezo kuwa hawakuona ugonjwa wowote, jambo lililosababisha hofu kutanda.
Akizungumza na waandishi wetu, mchungaji huyo alisema kutokana na kote huko kushindikana, aliamua kumchukua kijana huyo na kuishi naye nyumbani kwake kwa lengo la kumfanyia maombi.
Baada ya kumchukua, alianza dozi ya maombezi ya nguvu ambapo hivi sasa anaendelea vizuri.
Katika mahojiano na waandishi wetu, Pasco alisema hajui kilichotokea hadi akajikuta amefika Dar, tena getini kwa kaka yake akiwa uchi.
Alisimulia kuwa siku hiyo, alienda benki kutuma ada ya shule na baada ya hapo, alirudi nyumbani kwa bibi yake na kumkuta akiandaa ugali ambapo alikula kidogo kwani alikuwa akihisi maumivu makali ya kichwa.
Baada ya kushindwa kula vizuri, bibi yake alimtaka ale chungwa ambapo alichukua moja na kwenda nalo chumbani, akachukua panga kisha kulikata vipande viwili lakini alipoanza kula, kabla ya kumaliza kipande kimoja alihisi usingizi mzito ambapo alikuja kushtukia akiwa sehemu tofauti yaani getini kwa kaka yake akiwa amezingirwa na watu kibao.
Alieleza kuwa kutokana na kusumbuliwa na mauzauza ya kichawi ndiyo sababu kubwa iliyomfanya kaka yake amhamishie Rorya mkoani Mara ambako alienda kuanza kidato cha pili wakati huku Dar alikuwa ameshafika kidato cha nne.

Chanzo: GPL

Mishahara Mipya Serikalini, Angalia Ongezeko Lako Hapa.

-->
Madaktari Wakichapa Baada ya Ongezeko Hilo.

Serikali imetangaza mishahara mipya kwa watumishi wa umma itakayoanza kutumika mwezi huu, huku kima cha chini kikiongezwa kwa asilimia 41.18 kutoka Sh 170,000 hadi Sh240,000.
Vilevile, mishahara ya watumishi wengine wa umma imeongezwa kwa wastani wa asilimia 8.41. Waraka namba moja kwa watumishi wa umma uliotolewa na Katibu Mkuu, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, George Yambesi Julai 2 mwaka huu, unaeleza kuwa marekebisho hayo ya mishahara yatahusu watumishi wa serikali kuu na watumishi wa serikali za mitaa.

Wengine watakaonufaika na marekebisho hayo ni watumishi walioshikizwa kwenye taasisi za umma na watumishi ambao watakuwa kwenye likizo inayoambatana na kuacha kazi, kustaafu kazi au kumaliza mikataba baada ya Julai mosi mwaka huu.
Waraka huo umeonyesha kuwa watumishi wa serikali ambao wanapata mishahara binafsi isiyo ndani ya viwango vya mishahara ya serikali hawatahusika na marekebisho hayo.
Mei 29 mwaka huu, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, aliliambia Bunge, kwamba Serikali imekamilisha majadiliano ya kuongeza kima cha chini cha mshahara katika sekta 12 binafsi, kitakachoanza kutumika rasmi Julai mosi.

Waziri Kabaka alitaja sekta hizo kuwa ni ya Ujenzi, Shule Binafsi, Nishati, Viwanda na Biashara, Hoteli na Huduma za Majumbani, Ulinzi Binafsi, Madini, Afya, Uvuvi na Huduma za Majini, Usafirishaji, Mawasiliano na Kilimo. Kwa mujibu wa Kabaka, mishahara imepanda kwa kiwango cha asilimia kati ya 21 na 65 huku Afya ikiongoza kwa kuongezwa ikifuatiwa na sekta ya hoteli na huduma za nyumbani yenye asilimia 55.

Mei mosi mwaka huu akiwa mkoani Mbeya, Rais Jakaya Kikwete, aliahidi unafuu wa maisha kwa wafanyakazi kwa kuangalia uwezekano pia wa kupunguza kodi kwenye mishahara, Lipa Kadiri Unavyopata (PAYE).

Kuhusu kuongeza mishahara, Rais Kikwete aliahidi wafanyakazi wote kwamba Serikali itaendelea kuiongeza kulingana na hali ya uchumi wa nchi. Waraka huo unaonyesha kuwa mishahara mipya kwa watumishi wa serikali kada ya masharti (operational service), ngazi ya mshahara na mshahara mpya kwenye mabano ni;

TGOS A
TGOS A 1. (Sh240,000), TGOS A 2. (Sh245,600), TGOS A 3. (Sh251,200), TGOS A 4. (Sh256,800), TGOS A 5. (Sh262,400), TGOS A 6. (Sh268,000), TGOS A 7.(Sh272,000), TGOS A 8(Sh279,000), TGOS A 9.(Sh284,800), TGOS A 10(Sh290,400), TGOS A 11(Sh296,000), TGOS A 12(Sh301,600), TGOS A 13(Sh 307,200), TGOS A 14(Sh312,800), TGOS A 15(Sh 318,400), TGOS A 16(Sh324,000), TGOS A 17(Sh329,600) na TGOS A 18(Sh335,200).

TGOS B
TGOS B 1. (Sh347,000), TGOS B 2. (Sh356,500) TGOS B 3 . (Sh366,000), TGOS B 4 . (Sh375,500), TGOS B 5. (Sh385,000), TGOS B 6. (Sh394,500), TGOS B 7. (Sh404,000), TGOS B 8. (Sh413,500), TGOS B 9. (Sh423,000), TGOS B 10. (Sh432,500), TGOS B 11 . (Sh442,000) na TGOS B 12. (Sh451,500).

Inaendelea (Katika Chanzo) bonyeza Hapa

Cheka Upate Afya, Waionaje Tathmini hii ya Elimu ya Bongo?!!!

-->

Hapo Vipi Mjomba? Kwa Hali hii Tutafika Kweli?!!!!!!!!!!

"NGUVA" Wa Ukweli Avuliwa, Alimbembeleza Muhusika Amtunzie Siri ya Uwepo wake!!!

-->

Jumanne ya wiki hii huko Ibadan Nigeria, Mwanamke anayefahamika kama Ramota, ambaye ni muuzaji wa samaki wabichi ambao huvuliwa nakuwekwa katika mafriji alikutana na mkasa wa aina yake baada kukutana uso kwa uso na Samaki aina ya Nguva katika Moja ya Matenga ya Samaki aliyoyanunua.

Katika Harakati zake za Kuwatoa samaki hao na kuwapanga, Ramota alikutana na Samaki huyo mwenye Umbile na Nusu Mtu, Nusu Samaki, Hapo Mwanamke huyo alipiga kelele za kuomba msaada kwa majirani na akakimbia mbio kutoka nje.

Ramota alikimbia mpaka kwa Shehe mmoja wa maeneo ya Karibu ili aende kumsaidia, kutokana na kelele alizopiga na baada ya dakika chache kuonekana anarudi na Sheikh, watu walianza kujaa eneo la kazi la dada huyo.

Watu wachache walifanikiwa kumwona kiumbe huyo ingawa hawakupenda kuzungumzia zaidi ispokuwa mwanamke mmoja ambaye alikiri kumwona Nguva huyo na kwamba Ramota hakupaswa kupiga kelele wala kujaza watu kwani Samaki Mtu huyo alimwambia Asiseme kuhusu Kuwepo pale na kwamba alikuja kwa ajili ya kumnufaisha yeye.

Imeelezwa ya kwamba samaki mtu huyo alikuwa akiyasema maneno hayo huku akijificha na nywele zake zenye muundo wa rasta, huku akionekana kukamilika viungo vyote vya usoni licha ya udogo aliokuwa nao.

Kutokana na  zengwe la kujaa watu ilimbidi Ramota na Baadhi ya ndugu na Ma sheikh kumchukua Kiumbe huyo na kuondoka nae hapo kuelekea kwa Ndugu yao Mwingine.

Angalia Vizuri Picha aliyopigwa kupitia simu Kiumbe Huyo.



Nguva akimsihi asimtaje

Tathmini ya Vikao Vya Zabuni Serikalini na Taasisi Mbalimbali, Mtazamo wa Kipanya.

-->
Kama Picha Inavyoonesha, ni hali ya kuashiria jinsi gani mambo yalivyo siku hizi katika Vikao vingi vya Zabuni Aidha katika Halmashauri zetu au Taasisi Mbali mbali, Tutafika Tu.!!

 Image Credit: Kipanya.

Lulu Ajipanga Kurudi Darasani Tena


STAA wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekazia nia yake ya kutaka kurudi shule siku chache zijazo.
Lulu aliandika hayo juzikati alipokuwa akichati na mashabiki wake kupitia ukurasa wa facebook ambapo alikuwa akiulizwa maswali na kuyajibu live kupitia Runinga ya East Africa.
Mmoja wa mashabiki wake alimuuliza Lulu kuhusu mipango yake ya kurudi shuleni ambapo alimjibu kuwa yupo katika mipango  hiyo hivyo hivi karibuni atarudi darasani.
“Am on process..soon mpenzi nitarudi darasani,” aliandika Lulu ambaye awali alidaiwa kukatisha masomo yake ya sekondari.
Source: GPL
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga